Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewasili Songea Mkoani Ruvuma, leo tarehe 26 Februari 2026. Makamu wa Rais anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Tamasha la kumbukizi ya Miaka 120 ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji litakalofanyika tarehe 27 Februari 2026, Viwanja vya Makumbusho ya Majimaji, Songea.
Katika Uwanja wa Ndege wa Songea, Makamu wa Rais amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Hamad Chande , Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho, Viongozi mbalimbali wa Serikali, Taasisi, Dini, Vyama vya Siasa, Wananchi mbalimbali wa Ruvuma pamoja na Machifu wa kabila la Wangoni kutoka Afrika Kusini, Malawi na Tanzania.
Tamasha la Kumbukizi ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji, hufanyika mwezi Februari kila mwaka, likiwa na lengo la kuwakumbuka Mashujaa wa Tanzania waliopigana Vita vya Majimaji. Tamasha hilo la kihistoria linatarajiwa kuwa na shughuli mbalimbali za kitamaduni,maonesho ya historia pamoja na burudani zinazoakisi urithi na utamaduni wa wananchi wa kusini mwa Tanzania.










0 Comments