Header Ads Widget

KATIBU MKUU WA UMOJA WA MABUNGE DUNIANI (IPU) AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Bw. Martin Chungong, amewasili nchini katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, kwa ziara rasmi ya kikazi.

Lengo la ziara yake ni kutia saini Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya IPU na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufuatia uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukubali kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 153 wa IPU utakaofanyika Oktoba 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), jijini Arusha.

Hafla ya utiaji saini itafanyika Februari 27, 2026 katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam, ambapo Bw. Chungong atasaini makubaliano hayo pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, kwa niaba ya taasisi zao.

Aidha baada ya hafla hiyo, Bw. Chungong atafanya mazungumzo na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na IPU pamoja na maandalizi ya Mkutano wa 153 wa IPU.





 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI