Unguja – Zanzibar
Usafiri wa umma wa kutumia mabasi ya umeme Zanzibar unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Februari, 2026, ukianzia Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Mradi huu unaotekelezwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) unalenga kupunguza msongamano barabarani, kuboresha uhakika wa safari, na kuimarisha usafiri rafiki kwa mazingira.
Serikali kupitia ZSSF imeingia mkataba na Kampuni ya GRT Limited katika utekelezaji wa mradi huu, utakaotumia vituo vya kisasa na mfumo maalum wa uendeshaji katika barabara za kawaida.
Mradi huu utafanyika kwa awamu tatu, ambapo awamu ya kwanza itaanza Mkoa wa Mjini Magharibi kwa njia za:
Uwanja wa Ndege – Malindi
Buyu – Chukwani – Mnazi Mmoja – Malindi
Kituo cha Kijangwani kitatumika kama kiunganishi kikuu cha mabasi yote, sambamba na kuwepo kwa vituo ndani ya Uwanja wa Ndege na Bandari ya Malindi.
Mabasi ya umeme yanatarajiwa kuanza kuwasili mwanzoni mwa Februari, 2026.
Juhudi hizi za Serikali ya Awamu ya Nane chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa kuiletea Zanzibar maendeleo kupitia sekta mbalimbali







0 Comments