Header Ads Widget

WAZIRI MKUU AFUNGUA MKUTANO MKUU TAKUKURU, ASEMA SERIKALI IMEZIIMARISHA TAASISI ZAKE ZA UDHIBITI

 


Na Lilian Kasenene, Morogoroo 

Matukio DaimaApp 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba amesema Serikali imeendelea kuziimarisha na kuziongezea hari ya utendaji kazi taasisi zake zote zinazojihusisha na masuala ya udhibiti ikiwemo TAKUKURU.

Alisema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Mwaka wa viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU,uliofanyika mkoani Morogoro ambapo alimwakilisha Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

WaziriI mkuu Dkt Mwigulu alisema Serikali kila wakati imekuwa ikielekeza taasisi zake kuendelea kusimamia na kutoa huduma za kijamii,na utawala bora kwa wananchi ambapo aliwataka watanzania kuwa na utaratibu wa kufika katika ofisi za TAKUKURU kwa ajili ya kutoa taarifa na si akusubiri kuitwa tu panapotokea tatizo.


"Mheshimiwa Rais Samia si tu ameiiimarisha taasisi bali pia amezipa na ameziwezesha katika njanya mbalimbali ikiwemo vitendea kazi ili kufanya kazi kwa ufanisi,"alisema Waziri mkuu huyo.

Aidha akaitaka TAKUKURU kuimarisha vitendo vya ushirikiano ndani na nje ya taasisi hasa kwenye maeneo yenye hatari Rushwa ili Taifa liweze kuendelea.

Waziri mkuu Dkt Mwigulu akaipongeza TAKUKURU kwa kutoka fedha hizo ambapo zimetumika katika kufanya huduma za kijamii kwenye Elimu,Afya,Elimu bila malipo, barabara na madaraja maeneo mbalimbali nchini.


Aliitaka takukuru kushirikiana na sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma katika kuangalia namna ya kuboresha fomu ya tamko la maadili ya viongozi wa umma na kwamba isiwe kwa viongozi wa kisiasa na watendaji wengine wakuu bali iende katika ngazi na idara zinazohisika katika utekelezaji wa miradi inayotumia fedha nyingi za umma ikiwemo mikataba ya zabuni mbalimbali

"Nyie takukuru mna uzoefu wa maeneo yenye mianya ya Rushwa kwa maana fomu hiyo hawatalazimika kujaza fomu za utii ambazo hazimfanyi kuwajibika," alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Crispin Chalamila, awali akizungumza wakati wa mkutano huo alisema mkutano ni maalum kwa ajili ya kutathmini utendaji kazi wa TAKUKURU kwa madhumuni ya kujiimarisha na kuboresha utendaji kazi wao utakaowezesha kuimarisha pia mapambano dhidi ya rushwa. 


Aidha Chalamila alisema Rushwa ni tatizo la kidunia na lenye madhara makubwa kwa mtu mmojammoja, jamii, nchi na mataifa kwa ujumla,kwa sababu hiyo nchi zimeharamisha vitendo vya rushwa kuwa makosa ya jinai.

"Mkutano huu wa mwaka wa Viongozi wetu, hutumika kama jukwaa la kutathmini utendaji kazi wa TAKUKURU kwa kulinganisha na majukumu tuliyopewa kisheria," "Tathmini hii inatusaidia kubainisha mafanikio, changamoto, upungufu katika utendaji, fursa zilizopo pamoja na mbinu mpya za kuwezesha mapambano haya, ili kufikia lengo linalotajwa na Sheria"alisema Mkurugenzi huyo.

Pia alisema wanajivunia mafanikio mengi waliyoyapata katika miezi 12 ya mwaka 2024/25 na miezi sita ya mwaka 2025/26, ambapo alikiri kuwa mafanikio yametokana na juhudi na ushirikiano wa wadau wengine wa ndani na nje ya Tanzania.

Aliishukuru Serikali kwa kuiwezesha TAKUKURU kwa rasilimali watu, rasilimali fedha na vitendea kazi ambavyo vimechangia kwa kiasi kikubwa, katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi hata kufikia mafanikio hayo.

Mkurugenzi huyo alieleza kuwa TAKUKURU kwa miezi sita kati ya mwezi Julai na Desemba, 2025 imefanikiwa kuokoa zaidi ya Sh Bil 60.2 kupitia operesheni mbalimbali za uchunguzi,na fedha hiyo imerejeshwa Serikalini na nyingine kutumika katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kadiri ilivyokusudiwa.


TAKUKURU pia ilifuatilia matumizi ya fedha ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo 619 yenye thamani ya Sh Bil 553.45 na kufanikiwa kuokoa Sh Mil 173.5 zilizokuwa hatarini kupotea kwa njia za rushwa. 

Aidha katika kesi 489 zilizoendeshwa mahakamani, Jamhuri ilishinda kwa asilimia 68.8 kwenye kesi ambazo zilitolewa uamuzi na Mahakama ambapo washtakiwa walikutwa na hatia na kwamba imani yao kuwa kiwango hicho cha kushinda kesi kitaongezeka ifikapo Juni 2026.

Pia katika suala la udhibiti wa vitendo vya rushwa katika uchaguzi kwa nchi za SADC lilipewa kipaumbele ambapo TAKUKURU ilialikwa kujumuika katika timu za uangalizi wa uchaguzi,ambapo TAKUKURU iliweza kushiriki uangalizi wa uchaguzi wa Wabunge katika Jamhuri ya Mauritius, Uchaguzi Mkuu wa Botswana, na Uchaguzi Mkuu wa Msumbiji. 

Naye Waziri wa nchi ofisi ya Rais,menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Ridhiwani Kikwete alisema Serikali imeweza kuajiri watumishi wapya 980, huku alieleza kuwa Wizara itaendelea kusimamia taasisi zake kwa ukaribu ili kuleta ufanisi kwa watumishi.

"TAKUKURU katika Kila Wilaya zote nchini wamepatiwa gari Moja na ngazi ya mikoa wamepatiwa magari mawili naimani kwa kufanya hivyo hari na Mori zitaongezeka kwa watumishi,"alisema.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI