Header Ads Widget

WAKULIMA 1,065 WANUFAIKA NA UKUZAJI UJUZI.


Naibu Waziri Kisuo amesema Serikali yajipanga kuinua sekta ya Kilimo.

Mafunzo ya Ukuzaji Ujuzi yaleta tumaini jipya kwa Wakulima na Wasindikaji Wadogo

 Iringa

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Rahma Kisuo amefunga rasmi mafunzo ya ukuzaji Ujuzi kwa wakulima na wasindikaji wadogo 1,065 yaliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo kupitia Taasisi ya Kilimo Tanzania TARI.

Akizungumza leo tarehe 23 Januari 2026 wakati wa Hafla ya Kufunga Mafunzo ya Wakulima na Wasindikaji wadogo na Uzinduzi wa Mwongozo wa Uratibu Mafunzo ya Kuongeza Ujuzi kwa wafanyakazi, Mhe. Kisuo amesema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kutekeleza mkakati wa kuwawezesha wakulima na wasindikaji wadogo kwa kuwapatia ujuzi utakao wawezesha

kuongeza ufanisi na tija, kufanikisha ujasiriamali na kuwaongezea uwezo wa kibiashara wakulima hao.

Pia, amewapongeza washiriki wote 1,065 wa Mikoa ya Dodoma, Singida, Mbeya na Iringa kwa kushiriki mafunzo hayo na Kuwasihi watumie ujuzi walioupata kuinufaisha jamiii.

“Mkirudi maeneo ya kazi mkawe mabaloz wa mabadiliko pia nawasihi wakulima na wasindikaji wadogo nchini kushiriki mikutano, minada na maonesho yanayo andaliwa ndani na nje ya nchi ili kukuza shughuli za kilimo” Amesema.

Aidha ametoa Wito kwa wadau wa sekta ya Kilimo kuendeleza  ushirikiano kwa Serikali ili Sekta ya Kilimo kuwa na nguzo makini nchini.

Awali Akizungumza Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Ajira na Ukuzaji Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Bwa. Godwin Mpelumbe amesema serikali tangu mwezi Juni 2025 kupitia program hii Jumla ya watanzania 157,847 wamenufaika na Mafunzo ya Ukuzaji Ujuzi na Katika mwaka wa fedha 2026 serikali imetoa fedha kwa ajili ya programu ya kuongeza ujuzi kwa wakulima na wasindikaji Wadogo 1,065 huku Dodoma 261 Zao la Zabibu, Singida 258 katika zao la Alizeti, Mbeya 266 Zao la Parachichi , Iringa 250 Nyanya na Mchicha lishe.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Kilimo Tanzania Ni Bwa.Thomas Bwana. ameishukuru serikali kwa kuiamini TARI kuongoza Mafunzo hayo tangu yalipozinduliwa hadi kufika tamati siku ya leo.

Wakizungumza kwa nyakati tofaut wakulima na wasindikaji wadogo Bi. Noela Mapunda ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwa karibu na wakulima na kuwapatia mafunzo hayo ameiomba serikali iendelee kutoa mafunzo ya namna hiyo  kwa sababu imawaongezea uzalishaji, itaboresha kipato na kuchangia kikamilifu katika sekta ya kilimo na uchumi wa Kitaifa.





 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI