Header Ads Widget

WAJASIRIAMALI TARIME WAMSHUKURU RAIS SAMIA UJENZI WA SOKO LA KISASA


Wajasiriamali wa Soko kuu la Tarime Mkoani Mara lililogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 9.6 kutoka serikali kuu, wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa soko hilo, wakisema kwasasa wanafanya biashara zao katika mazingira salama, sahihi na tulivu, tofauti na ilivyokuwa hapo awali, suala linalowawezesha kupata faida zaidi katika Biashara zao.

Akizungumza kwa niaba ya wajasiriamali wengine leo Ijumaa Januari 23, 2026, Mjasiriamali Rebecca William amesema hakuwahi kutegemea kuwa Tarime wangepata soko kubwa na la kisasa kama hilo, akimuombea kheri na maisha marefu Rais Samia ili aweze kuwapelekea miradi mingine mingi zaidi ya maendeleo katika Wilaya yao.

"Nimefanya kazi kwenye soko hili kwa miaka minne, leo tunampongeza Rais Samia kwa kutujengea soko hili la kisasa na la Kimataifa, Mungu amlinde sana maana sisi Wakurya hatukuwahi kuota kuwa na soko kama hili lakini leo tumepata. Mama Samia hongera sana, Mungu akubariki." Amesema Bi. Rebecca.

Soko la Tarime ni miongoni mwa masoko mengine mengi yaliyojengwa na yanayoendelea kujengwa kote nchini, yakitajwa kuzingatia mahitaji ya kisasa ikiwa ni pamoja na kuwa na miundombinu imara, yakitajwa kukuza uchumi wa maeneo husika pamoja na kuongeza fursa za Watanzania kuweza kufanya biashara na kukuza vipato vyao kupitia biashara na kuongeza mapato kwa Halmashauri, suala linaloziwezesha Halmashauri kuweza kuhudumia wananchi.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI