Header Ads Widget

UZINDUZI WA MELI YA MV NEW MWANZA NI UTEKELEZAJI WA MAONO YA RAIS SAMIA- MWIGULU


Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema kuzinduliwa kwa Meli mpya ya kisasa ya MV New Mwanza katika Bandari ya Kusini leo Ijumaa Januari 23, 2026 ni dhihirisho la kuendelea kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kunakofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kama alivyoahidi kwa wananchi.

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu amebainisha hayo muda mfupo baada ya kuzindua meli hiyo, akieleza kuwa kuzinduliwa kwa usafiri huo ni tukio lenye kuonesha pia uwezo wa nchi katika kutekeleza miradi yake ya maendeleo.

"Tukio hili tunalolifanya leo la uzinduzi wa meli hii kubwa ni tukio linaloonesha uwezo wetu katika kutekeleza miradi ya maendeleo, linaelezea uwezo wa Kiongozi wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza maono makubwa yanayoweza kuwaletea Watanzania maendeleo." Amesisitiza Dkt. Mwigulu.

Meli hiyo iliyozinduliwa na Waziri Mkuu imejengwa na Mkandarasi kutoka Korea aitwaye Gas Entec Ship-building kwa kushirikiana na TASHICO, ikitengenezwa kwa teknolojia ya kisasa ikiwa ya ghorofa nne na ikiwa ndiyo meli kubwa zaidi katika Ukanda wa Maziwa Makuu, ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200, tani za mizigo 400, magari madogo 20 na magari makubwa 3 kwa wakati mmoja.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI