Header Ads Widget

TAASISI ZA PICTERUS AS NA GOAL 3 ZASHINDA RUZUKU YA EURO MILIONI 1 KULETA TEKNOLOJIA YA KISASA YA KUPIMA MANJANO KWA WATOTO WACHANGA TANZANIA


Taasisi za Picterus AS (Norway) na GOAL 3 (Uholanzi) pamoja wameshinda ruzuku ya Eurostars Euro milioni 1 (takribani Shilingi Bilioni 3 za Kitanzania) ili kuleta teknolojia mpya ya upimaji wa  manjano katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Kukiwa na uwezekano wa kusaidia mamilioni ya watoto  kuzuia matatizo makubwa ya kiafya yanayosababishwa na  manjano isiyotibiwa katika mazingira yenye rasilimali chache.

Taasisi hizo za Picterus AS (Norway) na GOAL 3 (Uholanzi) zinazofanya kazi nchini Tanzania kuunga mkono juhudi ya Serikali katika maboresho ya sekta ya afya wamekusudia kuboresha huduma za afya ya watoto wachanga, hasa kupitia teknolojia kwa kuleta teknolojia mpya ya kupima  manjano ya JaundiceCARE kwenye hospitali zenye uhitaji mkubwa nchini.


Lengo kuu likiwa kusaidia mamilioni ya watoto wachanga kutopata matatizo makubwa ya kiafya yanayosababishwa na  manjano kwa kutoa zana sahihi, nafuu, na rahisi kutumiwa na wafanyakazi wa afya zinazosaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga vinavyotokana na manjano. 

Teknolojia hiyo mpya ya programu ya simu (smartphone app) na kadi maalum inafanya uchunguzi wa ugonjwa wa  manjano kwa Watoto wachanga. 

Mradi huu unachangia katika Lengo la 3 la Maendeleo Endelevu la Umoja wa Mataifa (SDG 3) kwa kulenga kupunguza vifo vya watoto wachanga vinavyoweza kuepukika na kuimarisha usawa wa huduma za afya ulimwenguni kote. 

Teknolojia hii ya JaundiceCARE itawawezesha madaktari kupima watoto kwa kutumia simu janja (smartphone) bila kuhitaji kuchoma sindano.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI