Header Ads Widget

SERIKALI YAWEKEZA SH. TRILIONI 3 MIRADI YA MAJI, ASILIMIA ZAIDI YA 85 YA WANANCHI WAFIKIWA AWESO




 Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma


WAZIRI  wa Maji, Jumaa Aweso, amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewekeza jumla ya Shilingi trilioni 3 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji nchini, hatua iliyochangia kuimarika kwa upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi mijini na vijijini.


Aweso ameyasema hayo Januari 28, 2026 katika Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma, wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ahadi za siku 100 za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ameeleza kuwa kupitia uwekezaji huo, Serikali inaendelea kutekeleza miradi 878 ya maji vijijini pamoja na miradi 200 katika maeneo ya mijini, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha huduma ya maji inawafikia Watanzania wengi zaidi.



Aidha, Waziri Aweso amesema Wizara ya Maji imevuka lengo lililowekwa katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) la kufikia asilimia 85 ya upatikanaji wa maji ifikapo mwaka 2030, ambapo kwa sasa kiwango hicho kimefikiwa na kuvukwa, kikiwa zaidi ya asilimia 85 kitaifa.


Kwa mujibu wa Waziri huyo, jumla ya vijiji 10,758 tayari vimefikiwa na huduma ya maji katika maeneo ya vijijini na mijini, huku vijiji 1,575 vikibaki kufikiwa ili kufanikisha lengo la huduma ya maji kwa wote.


“Tangu Rais Samia alipoanzisha kauli mbiu ya ‘Kumtua Mama Ndoo Kichwani’, changamoto za upatikanaji wa maji zimepungua kwa kiasi kikubwa. Changamoto zilizobaki ni chache na Serikali imejipanga kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi, ili vijiji vyote vilivyosalia vipate huduma ya maji,”alisisitiza Aweso.


Ameongeza kuwa Rais Samia, kwa kutambua umuhimu wa maji katika maisha ya wananchi na maendeleo ya taifa, ameendelea kutoa kipaumbele kikubwa kwa sekta ya maji kupitia uwekezaji mkubwa wa Shilingi trilioni 3, unaolenga kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa uhakika na endelevu nchini kote.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI