Vijana nchini Tanzania wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa hatua kubwa za maendeleo zinazoendelea kupigwa kote nchini, pamoja na serikali yake kuwa sikivu katika kusikiliza na kufanyia kazi changamoto za wananchi hususani katika huduma za kijamii nchini.
Akizungumza na mwandishi wetu wa habari leo Ijumaa Januari 23, 2026, Bw. Denice Kirumba mkazi wa Tabata, Dar Es Salaam ameeleza matokeo chanya ya kuundwa kwa wizara ya maendeleo ya Vijana, akisema Wizara hiyo imemsaidia kutambua fursa mbalimbali za Vijana pamoja na kupata elimu ya namna ya kuweza kuwa mnufaika wake.
"Tunamshukuru sana Rais kwa kuunda Wizara hii ya Vijana kwani inasikiliza kero zetu, inatupa fursa mbalimbali na pia inatuelekeza kuhusu Mikopo na namna ya kuwa wajasiriamali."amesema Bw. Kirumba.
Kirumba pia ameeleza kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara za lami katika Mitaa mbalimbali, utatuzi wa kero za maji katika maeneo mengi nchini pamoja na ujenzi wa miundombinu mingine ya huduma za kijamii sambamba na maboresho yaliyofanyika kwenye utoaji wa huduma za afya na elimu kwa wananchi.






0 Comments