NA MATUKIO DAIMA MEDIA ,IRINGA
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeendesha semina maalumu ya maandalizi ya kustaafu kwa wanachama wake wanaotarajia kustaafu, iliyofanyika mkoani Iringa, kwa lengo la kuwajengea uelewa na kuwaondolea hofu kuhusu maisha baada ya ajira rasmi.
Kheri James RC Iringa ndie alipaswa kuwa mgeni rasmi .Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada, aliwashukuru viongozi wa NSSF kwa kuandaa semina hiyo muhimu na kuichagua Iringa kuwa mwenyeji.
Alisema semina hiyo ni fursa adhimu kwa wastaafu watarajiwa kujifunza namna bora ya kujiandaa kisaikolojia, kiafya na kiuchumi kabla ya kustaafu.
Mstahiki meya Iringa Ibrahim Ngwada mwakilishi wa RC katika mafunzo hayoMeya Ngwada aliwahimiza washiriki kushiriki kikamilifu katika semina hiyo ili kupata maarifa yatakayowasaidia kuishi maisha bora nje ya ajira rasmi.
Alisisitiza kuwa kustaafu ni neema na jambo la kujivunia, hivyo watumishi hawapaswi kuwa na hofu, bali wajipange mapema.
Aidha, alitoa wito kwa NSSF kuendelea kutoa elimu ya hifadhi ya jamii si tu kwa wafanyakazi wa sekta rasmi bali pia kwa wananchi waliopo kwenye sekta isiyo rasmi, wakiwemo wakulima, wafanyabiashara, wavuvi, wafugaji na bodaboda, akieleza kuwa makundi hayo nayo hufikia umri wa uzee na kuhitaji hifadhi ya jamii.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha MshambaKwa upande wake, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa NSSF, Robert Cosmas Kadege, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshamba, alisema semina hiyo ni sehemu ya utaratibu wa Mfuko wa kukutana na wanachama wake wanaokaribia kustaafu ili kuwapatia elimu kuhusu mafao ya pensheni, maandalizi ya kustaafu, fursa za kiuchumi baada ya kustaafu pamoja na kusikiliza changamoto zao.
Mwakilishi wa mkurugenzi mkuu akizungumza Meneja wa Huduma kwa Wateja wa NSSF, Robert Cosmas KadegeAliongeza kuwa Mfuko una dhamira ya kuwalinda na kuimarisha maisha ya wanachama wake tangu wanapokuwa kazini hadi wanapostaafu, akisisitiza kuwa wanachama ndio sababu ya uwepo wa NSSF.
Hata hivyo, Kadege alieleza kuwa Mfuko bado unakabiliwa na changamoto ya baadhi ya waajiri kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati au kutowasajili kabisa, na kutoa wito kwa waajiri kutimiza wajibu wao wa kisheria.
Semina hiyo pia imehusisha mada mbali mbali kutoka NSSF na taasisi za kifedha kuhusu umuhimu wa hifadhi ya jamii, maboresho ya huduma za NSSF, pamoja na huduma za kifedha zitakazotolewa na wawakilishi kutoka taasisi za kifedha, huku wastaafu watarajiwa wakipata fursa ya kuuliza maswali na kutoa maoni yao.
Washiriki wa Mafunzo hayo

.png)














0 Comments