Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma
LICHA ya Serikali ya awamu ya sita kuendelea kujenga Miundombinu Mizuri ya Barabara hapa nchini, Mbunge wa Jimbo la Moshi vijiji Mhe. Morris Makoi amekutana na kufanya Mazungumzo na Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega kuhusiana na Kusuasua kwa Miradi ya ujenzi katika Jimbo hilo.
Mhe. Makoyi ametaja barabara hizo ikiwemo barabara ya Rau Madukani- Mamboleo Materuni yenye urefu wa kilomita 9.99 ambapo urefu uliokamilika ni 2.9.
Akizungumza na Waziri wa Ujenzi Mhe. Ulega Mara baada ya kukutana na Kufanya Mazungumzo Mhe. Makoi amesema barabara hizo zimekuwa changamoto hivyo ni vyema serikali ikafanya mchakato kukamilisha ujenzi ili wananchi wapate Kutumia barabaraza hizo.
"Barabara ya chekereni-Kahe- Mabogini yenye urefu wa kilomita 31.25, kiboriloni- Mbokomu kilomita 14.34, Moshi International school- kibosho kati-Raphael kilomita 13.9, Samanga Chemchem kilomita 9.91, Mamboleo Shimbwe kilomita 10.3 pamoja na barabara ya Kidia road(usuduni-Kidia) kilomita 9.92". Amezitaja barabara hizo Mhe. Makoi.
Mara baada ya Mazungumzo hayo Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega amesema Serikali imeahidi kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa barabara Mbalimbali hapa nchini na barabara za Moshi vijijini zitajengwa kama dhamira ya Serikali ilivyokusudia.
Kukamilika kwa ujenzi wa barabara za Moshi vijijini kutarahisisha usafiri Pamoja na usafirishaji wa bidhaa na kuchochea shughuli za kiuchumi katika Jimbo la Moshi Vijijini.


.jpeg)




0 Comments