Na. Matukio Daima Media App, Dar
WAZIRI Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika usiku wa msimu wa Saba (7) wa Knockout Ya Mama, itakayofanyika viwanja vya Posta Kijitonyama, Dar es salaam, kuanzia saa 12 jioni Disemba 31, 2025.
Kwa mujibu wa waandaji wa pambano hilo, Mafiaboxing Promotion, wamebainisha kuwa, tukio hilo litashuhudiwa na wadau mbalimbali wa mchezo huo huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa, na viongozi wengine.
"Imebaki siku moja tu kuelekea usiku wa nguvu wa KNOCKOUT ya Mama utakaofanyika Desemba 31 katika Viwanja vya Posta Kijitonyama ambapo mabondia watapanda ulingoni kuwapa burudani kubwa ya kufunga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya kwa kishindo wapenzi wa ndondi kila bondia akijinasibu kuibuka na ushindi katika usiku huo.
Mashabiki wa ndondi mtaweza kushuhudia usiku huu kwa kihistoria mubasharakwa viingilio vya shilingi 10,000 Kawaida, 20,000 VIP na 50,000 VVIP au unaweza kufuatilia mubashara kupitia TV3 Sports HD king'amuzi cha Startimes chaneli namba 197 na TV3 Sports kingamuzincha Azam TV chaneli namba 416 pamoja na Mafia Online TV." Imeeleza taarifa hiyo ya Mafiaboxing Promotion.


.webp)
.webp)
.webp)
.webp)
.webp)
.webp)
.webp)
.webp)
.webp)





0 Comments