Takribani watu 19 wamefariki na 16 kujeruhiwa siku ya Jumatano baada ya majengo mawili kuporomoka huko Fez, mojawapo ya miji mikongwe zaidi Morocco, vimeripoti vyombo vya habari vya serikali.
Mamlaka za mkoa wa Fez ziliripoti majengo mawili ya karibu ya ghorofa nne yameporomoka usiku, limesema shirika la habari la serikali.
Majengo hayo yalikaliwa na familia nane na yalikuwa katika kitongoji cha Al-Mustaqbal.
Mara tu walipoarifiwa kuhusu tukio hilo, mamlaka za mitaa, idara za usalama na vitengo vya ulinzi wa raia walikwenda eneo la tukio na kuanza mara moja shughuli za utafutaji na uokoaji.
Fez, mji mkuu wa zamani katika karne ya nane na mji wa tatu wenye wakazi wengi nchini humo, ulikumbwa na wimbi la maandamano miezi miwili iliyopita dhidi ya serikali kutokana na kuzorota kwa hali ya maisha na huduma duni za umma.
Tovuti ya habari ya serikali ya SNRT imeripoti "kuwa majengo yaliyoporomoka yalikuwa na dalili za kupasuka kwa muda mrefu, bila hatua madhubuti kuchukuliwa."






0 Comments