Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
MADIWANI wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu wametakiwa kufuata Maadili ya Utumishi wa Umma ikiwemo kuwa waadilifu na kutokiuka maadili ya Utumishi wa Umma ili kuepuka mkinzano wa sheria.
Hayo yamesemwa na Afisa Maadili kutoka Ofisi ya Rais, Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Amasha Bura kwenye Baraza la kuapisha Madiwani wa Halmashauri hiyo kwenye ukumbi ulioko Nyaumata.
Bura amesema kuwa Madiwani wanatakiwa kujiepusha na Mgongano wa Maslahi ikiwemo kufanya Biashara au kandarasi mbalimbali na Halmashauri hiyo ili kuepuka kufanya kazi chini ya kiwango.
"Hauruhusiwi kuomba zabuni katika Halmashauri iliyopo sababu ikitokea umepata kandarasi na ukafanya Mradi huo chini ya kiwango, tutasimamiana?, tutamnyoshea kidole kiongozi huyo? hatuwezi kujisimamia...tuwe wazalendo na waadilifu kwa watumishi wa Umma" amesema.
Amewataka Madiwani hao kutumikia viapo vyao ili kuwa viongozi wa Mfano kwa wananchi ili kusimamia rasilimali na kuishi katika Mazingira ya Utumishi wa Umma.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga amewataka Madiwani hao kushirikiana ili kusukuma gurudumu la Maendeleo pia ni muhimu kuongeza juhudi ya kukusanya mapato.
Amewataka Madiwani hao kusimamia miradi ya Maendeleo kupitia Kamati za Madiwani walizounda ili zilete tija na matokeo kwa wananchi.
MADIWANI BARIADI MJI WAAPISHWA NA KJPEWA SOMO LA UADILIFU.
Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
MADIWANI wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu wametakiwa kufuata Maadili ya Utumishi wa Umma ikiwemo kuwa waadilifu na kutokiuka maadili ya Utumishi wa Umma ili kuepuka mkimzano wa shwria.
Hayo yamesemwa na Afisa Maadili kutoka Ofisi ya Rais, Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Amasha Bura kwenye Baraza la kuapisha Madiwani wa Halmashauri hiyo kwenye ukumbi ulioko Nyaumata.
Bura amesema kuwa Madiwani wanatakiwa kujiepusha na Mgongano wa Maslahi ikiwemo kufanya Biashara au kandarasi mbalimbali na Halmashauri hiyo ili kuepuka kufanya kazi chini ya kiwango.
"Hauruhusiwi kuomba zabuni katika Halmashauri iliyopo sababu ikitokea umepata kandarasi na ukafanya Mradi huo chini ya kiwango, tutasimamiana?, tutamnyoshea kidole kiongozi huyo? hatuwezi kujisimamia...tuwe wazalendo na waadilifu kwa watumishi wa Umma" amesema.
Amewataka Madiwani hao kutumikia viapo vyao ili kuwa viongozi wa Mfano kwa wananchi ili kusimamia rasilimali na kuishi katika Mazingira ya Utumishi wa Umma.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga amewataka Madiwani hao kushirikiana ili kusukuma gurudumu la Maendeleo pia ni muhimu kuongeza juhudi ya kukusanya mapato.
Amewataka Madiwani hao kusimamia miradi ya Maendeleo kupitia Kamati za Madiwani walizounda ili zilete tija na matokeo kwa wananchi.
Kupitia Baraza hilo, Madiwani hao walimchagua Nkenyenge Charles kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo baada ya kupata kura za ndio 14 huku Zawadi Mkilila akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kupata kura 14 za ndio.
Mwisho.

0 Comments