Header Ads Widget

WATANZANIA WAONYWA MILA ZINAZOHARIBU AMANI YETU

 

Askofu wa jimbo Katoliki Kigoma Mhasham Joseph Mlola akiendesha ibada ya Krismas iliyofanyika kitaifa katika Kotoliki Bikira Maria Mshindaji Kigoma

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

WATANZANIA wametakiwa kutokubali kuiga mila na tamaduni za kigeni ambazo zinapelekea kufanya mambo mabaya ambayo yamechangia katika kuharibu Amani yetu. 

Askofu wa jimbo Katoliki la Kigoma, Mhasham Joseph Mlola alisema hayo wakati wa ibada ya Krismas iliyofanyika katika kanisa Kuu la Bikiria Maria Mshindaji jimbo Katoliki Kigoma ambapo amesema kuwa ni lazima Watanzania wakatae kuiga mila na tamaduni za kigeni ambazo zinaharibu Amani, umoja na mshikamano wetu na badala yake kuilinda tunu hiyo ya Amani na umoja kwa nguvu kubwa.

Askofu Mlola alisema kuwa wakati waamini  wa kikristo duniani kote wakisherehekea kuzaliwa kwa Mtoto Yesu Kristo sherehe hizo ziende sambamba na Watanzania kubadilika na kuanza maisha mapya na kuondokana na mambo yote yaliyojitokeza na hivyo waishi kwa kupendana, kushikama na kuheshimiana kama ndugu huku akiwataka  kuvumiliana na kubebeana madhaifu yao.

Awali katika ibada ya Mkesha wa Krismas iliyofanyika kitaifa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Magharibi Askofu wa Dayosisi hiyo, Askofu Jackson Mushendwa aliwataka Watanzania kuipokea pasaka kwa roho ili kuwafanya kuishi katika Amani, upendo na mshikamano.

 Aidha katika ibada hiyo ya Mkesha wa Krismas Askofu Mushendwa amekemea tabia ya ushoga inayoshamiri nchini na kusema kuwa hali hiyo inatokana na kuiga tabia za nje na kuacha tabia na maadili ya Kitanzania na kiafrika ambayo yanazingatia misingi ya utu.


 Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI