Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima, Media, Dodoma
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Chamwino Mkoani Dodoma Kawea Kawea amesema si kweli kuwa wakulima wa mbogamboga na mazao mchanganyiko eneo la Bwigiri wanalazimishwa kulipwa fidia bila ya kufanya vikao vya makubaliano ili kupisha maeneo yao kama wanavyoelezea
Mwenyekiti huyo amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya wakulima wa eneo hilo kuulalamikia uongozi wa halmashauri kwa kuwataka wakulima hao kuondoka kwenye maeneo yao wanayoyamiliki ya kilimo kwa madai kuwa maeneo hayo yanatakiwa na halmashauri kwa ajili ya kuendelezwa kwa kuwapatia wawekezaji na kufanya kuwa mji wa halmashauri.
Kawea ameeleza kuwa halmashauri inataka maeneo hayo kuyaendeleza kwa kuujenga mji wa kisasa na kuweka wazi kuwa upimaji huo si wamabavu bali unaenda kwa vigezo vya ushirikishwaji na mwenye eneo anatakiwa kupimiwa na iwapo ataweza kulipia gharama za upimaji atapewa eneo lake na atakayeona kuwa hawezi ndipo halmashauri itampatia fidia.
"Sisi hatutaki migogoro na wananchi tunataka kupima maeneo yote na hela ya fidia ipo kwa walio tayari na kama kuna mtu ambaye anaweza kuripia gharama za upimaji atalipa na kupewa eneo lake,lakini zaidi ya yote mkulima ambaye hanaoana bado hajaelewa anatakiwa kufika ofisini Kitengo cha ardhi au kwa Mkurugenzi ili kupata maelezo zaidi kwani hayo ni maazimio ya baraza la madiwani"ameeleza Mwenyekiti halmashauri ya Chamwino.
Muda mfupi kabla ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kutoa ufafanuzi wakazi zaidi ya 1500 wa kata ya Bwigiri Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma, wanaoendesha kilimo chao cha mbogamboga,Matunda na kilimo mchanganyiko wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati mgogoro wa Ardhi kati ya wakulima hao na halmashauri ya Chamwino.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kuwa wanashangazwa na viongozi wa halmashauri kuwataka wakulima hao waondoke katika mashamba hayo kwa maelezo kuwa wamataka kupima maeneo hayo na kuweka mwekezaji mpya.
Mmoja wa wakulima na mmiliki wa mojawapo ya maeneo hayo Joram Jordan ameeleza kuwa imekuwa ni utamaduni wa viongozi kuzusha migogoro kati ya wakulima na Serikali jambo ambalo halijengi afya ya ustawi wa wakulima.
Mkulima huyo panoja na wengine kwa pamoja wameeleza kushangazwa kwao kwa kitendo cha viongozi wa halmashauri ya Chamwino kuwalazimisha wakulima hao kukubali kulipwa fidia ya shilingi Milioni 5 kwa heka jambo ambalo wanaeleza kuwa ni kutaka kuwajaza umasikini.
"Sisi kilimo ndo maisha yetu na tumezaliwa katika haya naeneo na tunaendesha maisha ya kusomesha watoto kwa kutegemea hii ardhi na ikumbukwe kuwa ardhi haiongezeki ila watu wanaongezeka.
"Hapa tumeisha anza kuandaa mashamba na serikali inahimiza sana kuwekeza katika kilimo lakini Serikali hile hile ya halmashauri inataka tuondoke je tutapata wapi sehemu ya kuishi kwa thamani hiyo ya Shilingi milioni 5"alihoji Jordan.
Naye Susan Makuka ambaye ameeleza kuwa ni mjane amesema yeye anaeneo muda mrefu sana na ndilo linalomsaidia kuendesha maisha na iwapo halmashauri itawalazimisha kuondoka kwa faida hiyo kiduchu ni mwanzo wa kufanya familia nyingi kuwa masikini.
"Sisi hatupingi upimaji au boreshaji lakini tunachotaka ni kupewa stahiki au fidia inayoendana ba ciwango vya sasa,leo hii maisha yangu ni ya kilimo nikitoa hapa na enda wapi na nitaanzia wapi kupata fedha za kuendeshea maisha ya familia yangu au wanataka kutufanya kuanza kundamana na kupigwa mabomu"ameeleza Susan.
Mwisho.








0 Comments