Header Ads Widget

WATANZANIA WANATAKA UWAZI NA UCHUNGUZI KAMILI- JAJI OTHMAN CHANDE


Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 Jaji Mkuu mstaafu Mohammed Chande Othman amesema Watanzania wanataka uchunguzi kamilifu wa Matukio ya Oktoba 29 pamoja na kutaka uwazi kwenye kutekeleza wajibu wao.

Jaji mstaafu Othman amebainisha hayo leo Jumatatu Disemba Mosi, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari, akisisitiza kuwa baadhi ya Mikutano yao wataifanya hadharani na mingine faragha ili kulinda haki za watu wengine.

"Mikutano yetu mingine itafanyika kwenye hadhara na mingine itabidi tuende kwenye faragha kwenye mazingira maalumu ili kulinda haki za mtu na Tanzania sasahivi tuna sheria ya kulinda faragha za watu." Amesema Jaji Othman.

Mwenyekiti huyo wa tume ameeleza kuwa matakwa hayo ya watanzania wameyapokea na ndiyo watakayoyatumia katika kujibu hadidu za rejea katika utekelezaji wa majukumu yao ya uchunguzi wa matukio hayo ya Oktoba 29, 2025.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI