Header Ads Widget

TUTAPONYA WAATHIRIKA WA MATUKIO YA OKTOBA 29, 2025


Jaji Mkuu mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 Mohammed Chande Othman amesema katika kutekeleza wajibu wa Tume hiyo, wanatarajia kuponya waathirika wa vurugu hizo pamoja na watuhumiwa wa matukio hayo ya Oktoba 29.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Disemba Mosi, 2025, Jaji Chande amesema watawatafuta walioshiriki, Vyama vya siasa, asasi za kiraia, wasimamizi wa uchaguzi na Tume huru ya Taifa ya uchaguzi, Viongozi wa dini na Watu wengine ili kuzungumza nao kuhusu matukio hayo.

Aidha pia ameeleza kuwa watazungumza pia na wajasiriamali, wafanyabiashara, watu mashuhuri, mamlaka za serikali za mitaa katika maeneo yaliyoathirika, Vyombo vya ulinzi na usalama, wanahabari na sekta binafsi pamoja na washirika mbalimbali wa maendeleo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI