Header Ads Widget

WAMILIKI WA MASHAMBA WALALAMIKIA BEI KUBWA YA UPIMAJI.


Na Matukio Daima Chamwino

WAKAzi wa kata ya Buigiri na Chamwino katika halmashauri ya Chamwino Mkoani Dodoma wameeleza kutoridhishwa na gharama za upimaji zinazotozwa kampuni ya upimaji inayojulikana kwa jina la  Company GREAT VISION LTD inayoendelea na zoezi hilo. 

Wakizungumza katika mkutano uliohitishwa na wananchi kwa lengo la kumtaka Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Tito Mganwa pamoja na watendaji wa halmashauri ili kutoa ufafanuzi jinsi ya gharama ya upimaji na utoaji wa fidia kwa wananchi wenyemaeneo katika eneo lililokusudiwa kupimwa.

Katika mkutano huo wamesema kuwa kuwa kitendo cha halmashauri kupeleka kampuni ili iweze kuwapimia bila kuwa shirikisha na kupanga bei ya pamoja ni kitendo cha kutaka kuwahujumu wananchi wenye maeneo hayo.

wamesema kuwa kampuni ambayo inapima maeneo haijakaa na wananchi kwa lengo la kufikia mwafaka.

Akichangia katika mkutano huo Mery Ndahani (74) amesema kuwa gharama ya upimaji ambayo inatozwa na kampuni hiyo nikubwa na haijakaa na wamiliki wa maeneo kupanga gharama halisi ya upimaji.

Mery ameeleza kuwa inaonesha kuwa mita za mraba moja kampuni inarakiwa kulipwa shilingi 1000 wakati huo Halmashauri haijaeleza italipa fidia kiasi gani cha fidia kwa wamiliki wa maeneo watakaopitiwa na miundombinu ya barabara au taasisi.

Mbali na hilo wananchi wameeleza dukuduku lao na kuwepo kwa historia ya wamiliki wa maeneo kupimiwa maeneo yao lakini hawalipwi fidia jambo ambalo wameeleza kuwa ni kuwarudisha nyuma kimaendeleo.

Pamoja na kuwepo na mvutano kati ya wananchi wanaomilili maeneo na Halmashauri ya Chamwino wametaka kusitisha zoezi la upimaji ili wananchi wakutane na kampuni ya upimaji ili kukubaliana bei rafiki ya upimaji kwani wamesema yakuwa hawakubaliani na kiwango cha sh.1000 kwa mita ya mraba moja.

Kwa upande wake Juma Sulu amesema kuwa wamiliki wa ardhi wanakubaliana na suala la upimaji na kupanga mji lakini hofu yao kutokuwa na uhakika wa kulipwa fidia kwa wakati kwani yapo madeni mengi bado hayajalipwa.

"Yapo maeneo mengi tumeruhusu kupimwa lakini mpaka saaa hatujalipwa lakini pia kwa sasa tunaendelea na kilimo zoezi linapofanyika kwa haraka hivi tutaendeshaje kilimo wakati mvua yenyewe ni ya kukimbizana.

"Lakini kwanini halmashuri hamtuambii wazi wale watakao pimiwa na kukutwa maeneo yao yapo katika miundombinu watafidiwa kiasi gani kwani hapa halmashauri imepigia fidia ya milioni 5 kwa heka moja huku mwananchi akilazimika kulipa shilingi 1000 kwa mita ya mraba moja ya upimaji"ameeleza Sulu.

Hata hivyo mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino Tito Mganwa ameeleza kuwa wananchi wote watapimiwa maeneo yao na hakuna hatakayepoteza haki yake.

Ameeleza kuwa ni hiari ya kila mmoja kulipia gharama ya viwanja atakavyo pata au kukubali kulipwa fidia pale atakapoona hawezi kulipia.

"Lengo la Serikali ni kuhakikisha mji wa chamwino unajengwa kwa mpangilio mzuri na majengo ya kisasa ili kila mmoja ajivunie kuwa chamwino ikiwa ni pamoja na kuharakisha huduma za kijamii" ameeleza Mkurugenzi.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI