Abdulkarim Mohamed, Mkazi wa Dar Es Salaam amesema kufanya vurugu kama sehemu ya kushinikiza serikali kutoa haki ama huduma fulani kwa jamii hakuna faida yoyote na badala yake vurugu zimekuwa sababu ya anguko la kiuchumi na kukwama kwa shughuli za kijamii na kiuchumi.
Mohamed amebainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea uzoefu na athari ya kiuchumi na kijamii aliyoipata wakati wa vurugu na matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akilaani wale wote walioratibu na kushiriki katika matukio hayo ya uvunjifu wa amani.
"Kwa mimi binafsi siliungi Mkono, sisi Tanzania tumezoea kuwa ni nchi ya amani na hao waliopanga jambo hili mapema kulingana na kauli zao hatukuamini kama jambo lile lingetokea na bado mpaka sasa tuna mashaka ikiwa kweli walikuwa ni Watanzania waliofanya matukio haya." Amesema Bw. Mohamed.







0 Comments