Header Ads Widget

CHRISTINE SOKOINE: WAZAZI TUWAFUNZE WATOTO MOYO WA KUJITOLEA, KUWA NA MAADILI MEMA




Na. Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

MDAU wa Elimu Nchini, Bi.Christine Towo Sokoine amewaasa Wazazi na Walezi kujenga utamaduni wa  kuwafundisha watoto maadili mema na kuwa na moyo wa kujitolea katika Jamii.

Bi.Christine Sokoine amesema hayo katika sherehe ya mahafali ya  15 ya Lavender Day Care Center (LDCC) iliyopo Bunju A, Jijini Dar  es salaam alipokuwa mgeni rasmi na kukutanisha Wazazi, Walezi, Walimu na wageni waalikwa kwa ajili ya kusherehekea safari ya ukuaji wa watoto wanaohitimu mwaka 2025.

Akitoa neno la shukrani kwenye mahafali hayo, Christine Sokoine amesema: Wazazi kuwafunza watoto Wahitimu kuwa na moyo wa kujitolea ikiwemo kusaidia watu, upendo na wema, lakini pia wakawe Mabalozi wazuri wa Levender.

"Muendelee kusoma kwa bidii hata mkitoka hapa, huko muendapo kwenye shule zingine mkawe mabalozi wazuri wa Lavender.

Mnapoenda kuanza dasara la kwanza, mkatumie vipawa vyenu mlivyofunzwa hapa.


burudani 


Meza kuu


Rai yangu kwa Wazazi na Walezi tuzingatie shule tunazopeleka watoto wetu, ikiwemo kuzingatia chaguzi sahihi za shule za msingi zinazo kidhi vigezo na maelekezo yanayotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na miongozo ya Taasisi ya Elimu Tanzania.

Vilevile, zinazozingatia ulinzi na usalama wa mtoto ili kuwaepusha na vitendo vya kikatili dhidi yao.Hii itasaidia kuwa na mwendelezo mzuri wa msingi ambao watoto wameupata wakiwa hapa Lavender." Amesema.

Lakini pia nimpongeze Mkurugenzi wa Lavender kwa namna ya kipekee kuendeleza kituo hiki ikiwemo kuongeza majengo mapya na kuanzisha kupokea watoto wa miezi Sita wataanza kupokelewa hapa kuanzia 2026.

Tunafahamu changamoto za Walezi wa watoto siku hizi, hili ni jambo jema sana.

Kuhusu vipaji mnavyofundisha: "Watoto wakiwa na kipaji mfano Piano ama uogeleaji, vitasaidia kupata ajira ya ziada na vitamsaidia Mtoto kwenye mahitaji yake na hata pia kupata mashindano ya kuzunguka nchi mbalimbali kwenye mashindano." Amesema Bi.Christina Sokoine.





Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kituo cha Lavender Day Care, Bi.Vida Andrew Ngowi amewashukuru Wazazi na Walezi kwa kuendelea kuwaunga mkono na kwa sasa wanaendelea kuongeza majengo mengine ya Kituo hicho.

"Tuna fahamu kuna changamoto ya malezi kwa baadhi ya wadada wa kazi, Mnaweza kuanza leta watoto wenu wa kuanzia miezi Sita hapa Lavender. Utaratibu ni  Wazazi mnawaleta wenyewe hapa shule asubuhi na kuja kuwachukua jioni (kituo kinakuwa wazi asubuhi hadi Saa 12 jioni), 

"pande huu ni nimebobea hivyo karibuni sana Wazazi wote kuwaleta watoto wenu." Amesema Mkurugenzi Bi. Vida Ngowi.

Nae Mkuu wa kituo hicho cha Lavender, Bi. Agnes Joseph Njau kupitia risala yake amesema Lavender ilianzishwa mwaka 2010 kwa lengo la kutoa huduma bora ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto. 





"Kituo kilianza na watoto wachache mwaka 2010 na hadi kufikia sasa tuna watoto wengi, tuna washukuru Wazazi na Walezi kutukimbilia Lavender.

Lakini pia katika kuzingatia ubora wa kituo, kumekuwa na ongezeko la vifaa, michezo na vitabu vya watoto lakini pia  kupata mtaalamu kila mwaka kutoka Ujerumani  kwa ajili ya kufundisha Walimu, hivyo Walimu wetu wana umahiri mkubwa katika malezi ya kufundisha watoto.  

"Kituo cha Lavender kina tawi katika eneo la Kitunda Masai ambacho nacho kinafanya vizuri sana, Kituo chetu watoto wanajifunza kifaransa, kuogolea na muziki kama chaguo kwa wale wanaopenda. 



Mkuu wa kituo hicho cha Lavender, Bi. Agnes Joseph Njau akisoma risala katika sherehe hizo





Wanafunzi wahitimu wa kituo cha Lavender wakikata keki






Mdau wa Elimu Nchini, Bi.Christine Towo Sokoine akimkabidhi cheti mmoja wa Wahitimu wa elimu ya awali wa kituo cha Lavender Day Care katika mahafari ya 15, yaliyofanyika November 29,2025, Bunju A,


Mkurugenzi wa kituo cha Lavender Day Care, Bi.Vida Andrew Ngowi akitoa neno


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI