Khalid Malecha, Mkazi wa Kitonga Jijini Dar Es Salaam, ameeleza kuwa maelfu ya wananchi waliathirika moja kwa moja na ghasia na matukio ya uvunjifu wa amani uliojitokeza Oktoba 29, 2025, akihamasisha Jamii kuienzi amani ya Tanzania na kufuata taratibu rasmi za maandamano.
Malecha amebainisha hayo leo Alhamisi Disemba 04, 2025 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, akionesha pia kusikitishwa na waliofanya vurugu hizo kukosa sababu za msingi za kufanya hivyo.
"Tuangalie zaidi amani tuliyo nayo katika nchi yetu kwasababu tuna mengi tunayotaka kuyafanya kwente maisha yetu hususani Vijana wenzangu ikiwemo malengo tuliyonayo kwani fursa zipo nyingi ambazo Rais wetu ametuwekea." Amesema Bw. Malecha.
Malecha amezungumzia pia matarajio yake katika Wizara mpya ya maendeleo ya Vijana, akisema anaamini kupitia Wizara hiyo Vijana watazifahamu fursa nyingi zaidi za kiuchumi na ajira, suala ambalo litawatoa Vijana katika hatua moja kuelekea nyingine katika ukuaji wa uchumi.







0 Comments