Header Ads Widget

SERIKALI KUFANYA MAGEUZI YA UONGOZI LA SHIRIKA YA UMMA, UTEUZI 2026 KUFANYIKA KWA USHINDANI


SERIKALI imepanga kufanya mageuzi kabambe katika uongozi wa mashirika ya umma, ikiwemo kuhakikisha watendaji wakuu na wajumbe wa bodi wanateuliwa kupitia mfumo wa ushindani wa wazi ili kuongeza uwazi, uadilifu na ushiriki mpana wa Watanzania wenye sifa stahiki.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema mfumo huo mpya utaanza kutumika rasmi kuanzia Julai 1, 2026, mara baada ya sheria mpya inayoandaliwa na Serikali kupitishwa.

Amesema hatua hiyo ni sehemu ya mpango mpana wa kuboresha utendaji wa mashirika ya umma, kuondoa utaratibu wa uteuzi wa moja kwa moja, na kujenga imani ya wananchi kwa kuweka mazingira ya ushindani wa wazi kwa nafasi zote za uongozi.

“Kama ni Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO utaomba na utashindanishwa. Ukihitaji kuwa mjumbe wa bodi ya TPA au TISEZA utapitia mchakato wa ushindani. Watanzania wote wenye sifa wataomba, na uteuzi utafanywa kwa competitive recruitment,” amesema Prof. Mkumbo.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Waziri Mkumbo alisema mageuzi hayo yanaenda sambamba na hatua za kuongeza ufanisi wa mashirika ya umma ili yaweze kuchangia kikamilifu kwenye uchumi wa taifa na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Amebainisha kuwa Serikali inaunda mfumo mpya wa kupima utendaji wa mashirika hayo kwa kuzingatia tija ya kiuchumi na ubora wa huduma kila shirika litapewa vigezo vipya vya kupimwa, na tathmini yake itahusisha mchango wake katika kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Aidha, sheria mpya itayataka baadhi ya mashirika ya umma ya kibiashara kujisajili katika Soko la Hisa, hatua itakayowezesha Watanzania kununua hisa na kumiliki sehemu ya mashirika hayo hatua hiyo inalenga kupanua uwazi, kuongeza uwajibikaji wa menejimenti na bodi, na kuvutia uwekezaji mpana kutoka kwa wananchi.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI