Na Matukio Daima App
Mbeya
MWANAMKE Mmoja aitwaye ,Marry Timotheo mkazi wa kijiji cha Garijembe kata ya Tembela Wilaya ya Mbeya anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga na kitu kizito kichwani mtoto wake ,Scola Mwaba(10)kwa madai ya kuzidi utukutu kisha mwili wake kutupa shamba lilo karibu na nyumbani anakoishi .
Akizungumzia tukio hilo Desemba 10,2025 Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema marehemu Scola alikuwa Mwanafunzi wa Darasa la Nne shule ya Msingi Ngonde wilaya ya Mbeya.
Kuzaga amesema kuwa tukio hilo limetokea Desemba 9,2025 ,majira ya saa 6.30 mchana katika Kijiji cha Garijembe ,Kata na Tarafa ya Tembela Wilaya ya Mbeya.
"Mama wa marehemu alimshambulia kwa kitu kizito kichwani mtoto wake kwa madai ya kuzidi utukutu kisha mwili wake kutupa jirani na shamba la nyumba anakoishi "amesema Kamanda Kuzaga.
Aidha Kuzaga ameeleza kuwa pia licha ya kumshikilia mama wa marehemu ,pia jirani yake ,Sharifa Nzalanje anashikiliwa na Polisi baada ya kuhusika kushirikiana katika tukio hilo.
Hata hivyo amesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha tukio hilo ni kujichukulia sheria mkononi kumuadhibu marehemu kwa kumpiga hadi kufa na kisha mwili wake kutupa shambani jirani na nyumba wanaoishi.
Kuzaga amesema kuwa baada ya kubaini kuwa marehemu amefariki dunia mama mzazi kwa kushirikiana na jirani yake walienda kutupa mwili wake shambani .
Amesema kuwa watuhumiwa wanaendelea kushikiliwa na upelelezi ukikamilika hatua za kisheria zitachukuliwa.
Kamanda Kuzaga ametoa wito kwa wazazi na walezi kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mkononi kwa kuadhibu watoto badala yake watoe adhabu za kuwarekebisha kuwafundisha mienendo ya maadili mema.
Pia amezitaka jamii kuwa mabalozi wa kutoa taarifa za wazazi na walezi wanaofanya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ili hatua za kisheria zichukuliwe na kuhepuka madhara yanayoweza kuwapata ikiwepo kupoteza maisha au ulemavu wa kudumu.
Fatuma Idrisa ni mkazi Inolo wilaya ya Mbeya amesema kuwa ipo.haja kwa wazazi na walezi kuacha kutumia vipigo vilivyo pitiliza kwa watoto wao pindi wanapokuwa na changamoto za kifamilia hivyo hasira kumalizia kwa watoto.






0 Comments