Na Matukio Daima App Kibaha
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kibaha imetenga kiasi cha shilingi milioni 900 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mapya kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaotarajiwa kujiunga mwaka 2026.
Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dkt. Nicas Mawazo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano Halmashauri ya Manispaa hiyo.
Mawazo amesema kuwa wanafunzi waliofaulu darasa la saba mwaka huu ni 6,000 sawa na asilimia 100 hivyo wamejipanga wanafunzi wote kutopata changamoto ya miundombinu ya madarasa na madawati.
Amefafanua kipindi kilichopita wanafunzi walifaulu 3,050 hivyo kwa mwaka huu idadi imeongezeka kwa kiasi kikubwa.
mwisho.







0 Comments