Header Ads Widget

NJALU AWATAKA MADIWANI KUSHIRIKIANA KULETA MAENDELEO ITILIMA.


MBUNGE wa Jimbo la Itilima, Njalu Silanga akizungumza kwenye Kikao cha kuwaapisha Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Itilima.


Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima.


MBUNGE wa Jimbo la Itilima, Njalu Silanga amewataka Madiwani kushirikiana na Serikali kuhakikisha wanawatumia wananchi hasa kusimamia miradi ya Maendeleo kutokana na fedha zinazoletwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.


Akizungumza kwenye baraza la kuapisha Madiwani, lililofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Itilima, Njalu amewasisitiza Madiwani na watumishi kushirikiana kusukuma gurudumu la Maendeleo.



"Waheshimiwa madiwani wenzangu tumepata Dhamana hii siyo kwamba sisi ni bora zaidi ya wengine bali tumeaminiwa kuwa sauti ya wananchi wenzetu tushirikianeni, tupendaneni na jukumu letu kubwa liwe kuijenga Itilima yetu kwa kusimamia vizuri pesa zinazoletwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwaajili ya maendeleo.Ninawaomba sana ndugu zangu tujikite katika kuleta majawabu na siyo madiwani tunaoshinda polisi ili miaka mitano ikiisha tuwe na ujasiri wa kuonyesha tuliyoyafanya" amesema Njalu.

Daudi Nyalamu ameibuka mshindi katika nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kupata kura 31 kati ya kura 31 zilizopigwa huku Mboje Mhuli akichaguliwa kuwa makamu Mwenyekiti kwa kura 31 kati ya kura 31 zilizopigwa.

Mwisho. 








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI