![]() |
| Mkurugenzi Mtendaji wa F&M Global Ltd (Creative Agency), Bw. Fadhili (katikati) akiwa na tuzo hiyo aliyopoka kwa niaba ya ZARA Tanzania Adventures |
Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam.
MKURUGENZI Mtendaji na Mwanzilishi wa ZARA Tanzania Adventures (ZARA TOURS), Bi. Zainab Ansell "Mama Zara" ametunukiwa Tuzo ya Wanawake 100 wenye nguvu zaidi katika Biashara Afrika Mashariki.
Tuzo hizo zimetolewa Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki, Desemba 2025,
Awali akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya ZARA Tanzania Adventures, Mkurugenzi Mtendaji wa F&M Global Ltd (Creative Agency), Bw. Fadhili ameshukuru kupokea tuzo hiyo kwa niaba ya ZARA Tanzania.
![]() |
| Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa ZARA Tanzania Adventures (ZARA TOURS), Bi. Zainab Ansell "Mama Zara" |
"Ninashukuru kwa fursa hii ya kipekee na ninajivunia kupokea tuzo hii ni kielelezo cha dhamira yetu ya kujituma na ubora katika sekta ya utalii na ukarimu.
Tunaiweka tuzo hii kwa mashabiki na wateja wetu wote, kwa sababu bila ninyi, ZARA isingekuwepo. Asanteni sana, na upendo mwingi kwa wateja wetu wa ndani na wa kimataifa.
Asante Mama Zara, Asanteni timu nzima ya ZARA Tanzania Adventures kwa kutambua juhudi zetu na kwa msaada wenu wa kila wakati." Ameeleza Fadhili.
Na kuongeza kuwa, Imani aliyoipa kampuni ya F&M Global Ltd, ni heshima kubwa kumwakilisha yeye pamoja na timu nzima ya ZARA Tanzania Adventures katika Masuala ya Uhusiano wa Umma na Masoko kwenye tukio hilo kubwa nchini.
![]() |
| Mkurugenzi Mtendaji wa F&M Global Ltd (Creative Agency), Bw. Fadhili akiwa na tuzo hiyo aliyopoka kwa niaba ya ZARA Tanzania Adventures |










0 Comments