Mkuu wa kitengo cha wafanyabiashara wadogo na wa kati kutoka Eco bank Bwana Juma Hamisi akiongea na waandishi wa habari
NA NAMNYAK KIVUYO,MATUKIO DAIMA MEDIA, ARUSHA
Tasisi ya kifedha ya Eco bank imekuja na nia ya kuunga mkono taasisi za kielimu kwa kuanzisha huduma maalum za akaunti za shule zisizokuwa na makato pamoja na ulipaji ada kupitia contro namba.
Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano mkuu wa 20 wa wakuu wa shule za sekondari Tanzania, Mkuu wa kitengo cha wafanyabiashara wadogo na wakati kutoka eco bank Juma Hamisi alisema kuwa wameamua kuingia upande wa elimu kwakuwa wanaamini elimu ndio silaha namba moja ya kupigana na umasikini.
"Tumekuja na akaunti sizizo na makato yoyote kama mchango wetu wa Elimu Tanzania lakini pia mfumo wa kutoa taarifa baina ya mzazi na shule wakati wa ulipaji ada(contro namba) ikiwa ni pamoja na utoaji wa mikopo wa midogo, mikopo ya muda mfupi pamoja na mikopo ya muda mrefu kwalengo la kuendeleza ujenzi wa shule au kununua vifaa vya shule," Alisema.
"Bila tasisi za fedha kuna vitu vingi vinarudi nyuma au vinakosa maendeleo kwahivyo tumeona tuwekeze kwenye elimu kwasababu ndiyo iliyomfanya kila mmoja wetu kusimama mahali hapa leo hii itasaidia kutokuzorota kwa elimu,"Alieleza
Aidha aliendelea kusema kuwa bila elimu wanaweza wakawa na mali lakini bila elimu hawataweza kusimamia ipasavyo na ndio mana ECO Bank ikawa mstari wa mbele kuhakikisha wanasapoti mambo yanayohusiana na elimu.
"Na tumeona kuna umuhimu wa kuwekeza katika kufanikisha mkutano huu kwasababu foram zinazokutanisha watu wengi zinakupa fursa ya kuweza kuzungumza na watanzania wote juu ya utatuzi tulionao kuhusu changamoto mbalimbali za kielimu," Alifafanua.
Awali akifungua mkutano huo Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) Profesa Riziki Shemdoe wakati akifungua mkutano huo mkoani Arusha aliwataka wakuu wa shule za sekondari kwenda kusimamia na kukomesha utoro wa walimu na wanafunzi mashuleni kwani jambo hilo bado linathiri usimamizi wa ufundishaji na ujifunzaji.
"Ufundishaji unategemea uwepo wa walimu na wanafunzi na endapo itatokea mwalimu hayupo basi ataathiri ufundishaji na ukamilishaji wa mada zilizopanga hivyo hivyo kwa mwanafunzi lakini pia kasimamieni nidhamu na kudhibiti utoro kwa walimu na wanafunzi shuleni lakini pia
Simamieni utokomezaji wa vitendo vya ukatili kwa wanafunzi na kuzuia mimba kwa wanafunzi wa kike kwa kuboresha madawati ya ushauri na unasihi pamoja na ulinzi na usalama wa mtoto," Alisema Profesa Shemdoe.








0 Comments