Mbunge wa jimbo la Kilolo, Dr. Ritta Enespher Kabati amewataka Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kuchangamkia fursa ya mradi wa ng'ombe wa maziwa.
Kabati ameyasema hayo wakati wa mkutano wa wananchi pamoja na waratibu wa mradi wa mageuzi ya tasnia ya maziwa na mabadiliko ya tabia ya Nchi uliofanyika katika kata ya Mtitu, kijiji cha Luganga.
Amesema mradi huo ni mahususia kusaidia Wananchi kiuchumi pamoja na kupambana na suala la lishe kwa kuongeza upatikanaji wa maziwa.
Kabati amewasihi vijana, wanawake na makundi maalum kujiandaa kikamilifu kupokea mradi huo kwa awamu ya kwanza ukianza katika kata ya Mtitu, Ng'uruhe na Image.
Akizungumza wakati wa kuutambulisha mradi, mratibu wa mradi huo Goodluck Massawe amesema mradi wa ng'ombe wa maziwa ni wa miaka 10 huku ukianza katika mikoa 8 ya Tanzania na wilaya 3 za mkoa wa Iringa.
Ameongeza kuwa mradi huo utahusisha kupatiwa ng'ombe wa maziwa bure kwa wananchi wa kaya maskini pamoja na mkopo kwa gharama nafuu kwa wananchi wenye kipato nafuu.
Aidha wanufaika wote wakipatiwa mafunzo na nyenzo mbakimbali kuhakikisha ufanisi wa mradi.










0 Comments