Header Ads Widget

MAHAFALI YA 6 YA LAVENDER DAY CARE CENTER YAFANA KITUNDA MASAI

 


Na. Mwandishi Wetu, Dar.

MAHAFALI ya sita (6) kwa Watoto wa darasa la Awali ya Kituo cha Lavender Day Care Center kilichopo Kitunda Masai, yameweza kukonga nyoyo Wazazi na viongozi waliofika kushuhudia tukio hilo la kipekee katika kuhitimisha Wanafunzi hao.

Katika mahafali hayo yaliyofanyika hivi karibuni Disemba 2025, Wahitimu hao wa darasa la awali wameweza kuonesha uwezo wao mkubwa wa yale waliofundishwa darasani kama masomo na michezo mbali mbali.

Awali mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mdau wa Elimu Bi. Elly Kitaly ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi ya Chadron's Hope Foundation amepongeza uongozi wa shule, Walimu pamoja kwa namna ya kipekee katika kumsaidia Mtoto kitaaluma sambamba na wazazi kwa kuichagua Lavender Day Care tawi la Kitunda Masai.




Amesema uwezo wa watoto hao ni mkubwa hivyo wanatakiwa kuendelea kusimamiwa katika malezi sahihi ya kielimu na kuendelea kujengwa katika mambo mema katika hatua ya Elimu ya Msingi.

Bi.Elly Kitaly amesema kuwa, Elimu ni muhimu lakini pia vitu vingine vya Msingi kabisa vinapaswa kufundishwa Watoto ilikuwajenga zaidi.

"Nimeona kuna watu wana elimu kubwa lakini hawafanyi mambo makubwa.Elimu ni pamoja na mambo ya msingi ni kwa kujifunza Hutu, kujifunza kuwa mkweli na kujifunza kusimama kwenye haki." Amesema Bi. Elly Kitaly.

Aidha, katika risala ya Kituo hicho, juu ya kuongeza majengo mengine, Bi. Elly Kitaly amesema kuwa anaamini Wazazi wanaweza kuchangia chochote ilikufanikisha ujenzi huo kwani itasaidia maendeleo ya watoto wengi.

"Nimesikia tunataka kujenga majengo mengine, moja ya changamoto ya kuendeshea shughuli kama hizi za taasisi za shule ni suala la kifedha, na nafahamu pesa ni changamoto hivyo tuungane kusaidia kituo cha Levender ili kiendelee kusaidia watoto wetu, Mimi na wewe tuungane tukatoa kilichopo mifuko ya cement, au matofali au hata kuchangia elfu moja (Tsh 1,000) inaweza kubadilisha mazingira ya Lavender.




Ameongeza "Utakuja hapa utakuta mazingira safi yame boreshwa, madarasa yame ongezeka, sehemu ya michezo ya watoto imeboreshwa hata utakuta na eneo la kuogelea (swimming pool) ya watoto.

Aidha amesema kuwa, Elimu ni muhimu, lakini pia lazima tujifunze mengine kama fani ya muziki, kuogelea na mengine katika vipaji ili kukabiliana na soko la ajira.

"Nimeona watoto wamefanya mambo makubwa hapa, niwapongeze Uongozi wa Lavender, na Walimu kwa kuwalea vyema watoto hawa, na wakawe mfano huko katika ngazi inayofuata.




Nae Mkurugenzi wa kituo cha Lavender Day Care, Bi.Vida Andrew Ngowi amewashukuru Wazazi na Walezi kwa kuendelea kuwaunga mkono na kwa sasa wanaendelea kuongeza majengo mengine ya Kituo hicho cha eneo la Kitunda Masai.

Aidha, kupitia risala ya msimamizi wa kituo hicho, amesema Lavender Day Care Center kilichopo Kitunda Masai ilianzishwa mwaka 2019 kwa lengo la kutoa huduma bora ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto. 

"Kituo kilianza na watoto wachache mwaka 2019 na hadi kufikia sasa tuna watoto wengi, tuna washukuru Wazazi na Walezi kutukimbilia Lavender kwa hapa eneo la Kitunda Masai, kwani kituo chetu "Mtoto ndiye kiini cha ujifunzaji ", lakini pia falsafa yetu kuu inasema"Tunajifunza kupitia michezo".




Kituo cha Lavender pia kina tawi katika eneo la Bunju A ambacho nacho kinafanya vizuri sana ikiwemo watoto wanajifunza kifaransa, kuogolea na muziki kama chaguo kwa wale wanaopenda. 























Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI