Na,Jusline Marco;Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Joseph Modest Mkude leo Desemba 25 ,2025 akiwa katika Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Theresi wa Mtoto Yesu,Jimbo Mkuu Katoliki Arusha amewakumbusha wazazi wa Mkoa wa Arusha kuweka akina ya fedha kwaajili ya kuwapeleka watoto wao shule ifikapo januari 2026.
Akizungumza baada ya kumaliziaka kwa Misa Takatifu ya Kiaskofu iliyofanyika katika Kanisa hilo,Modest amewataka wazazi na walezi katika kusheherekea sikukuu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo na sikukuu ya Mwaka mpya wapokee pia majukumu yao yanayoanza mwaka 2026.
Aidha amewasisitiza wananchi wa Mkoa wa Arusha katika kusheherekea huko wajiandae kupokea mambo mbalimbali kama vile elimu ambapo pia amesema ofisi yake imejipanga kutoa Elimu ya afya ya bima kwa wote kwa wakazi wa Jiji la Arusha kutokana na wengi wao kutokuwa na elimu juu ya bima hiyo.
Kulingana na mahubiri ya leo,Modest ametumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha wakazi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla kuendelea kulinda amani na kuiombea nchi sambamba na kuwa na upendo kwenye familia zao na kuepuka kufanya mambo yanayoiharibu jamii ikiwemo ulevi na uvutaji wa bangi.








0 Comments