NA MATUKIO DAIMA MEDIA.
IRINGA.
Mahakama kuu kanda ya Iringa katika kuadhimisha miaka 20 ya mahakama hiyo wanajivunia kupunguza kwa kiasi kikubwa mlundikano wa mashauri kwa kutekeleza kampeni maalumu ya kuondosha mashauri yaliyokaa muda mrefu mahakamani.
Akizungumza na wanahabari leo Disema 5, 2025 Jaji Mfawidhi mahakama kuu kanda ya Iringa Dunstan Ndunguru alisema maadhimisho hayo yanatarajia kufanyika disemba 15, 2025
Jaji Ndunguru alisema kuwa wamefanika kwa kufuatilia mwenendo ya mashauri na kuhimiza matumizi mbadala ya utatuzi wa migogoro na matokeo yake ni kupungua kwa mashauri yaliyokwama na kuongeza kasi ya utoaji maamuzi.
Alisema kuwa lengo la kuzungumza na wanahabari ni kuweleza umma juu ya maadhimisho ya miaka 20 ya mahakama kuu kanda ya iringa yenye kauli mbiu “safari ya miaka 20 ya mahakama kuu”
“Tunaendelea kusisitiza uwazi,uwajibikaji na utoaji wa huduma kwa heshima na weledi, huku huduma za kutoa taarifa zimeboreshwa na wananchi wanaendelea kupewa elimu juu ya mwenendo wa mashauri na taratibu za mahakama”alisema
Jaji Ndunguru alisema kuwa pamoja na mafanikio hayo bado wanakabilia na changamoto kama vile wananchi kutoelewa taratibu na utendaji kazi wa mahakama, wananchi kutokuelewa umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi.
Alisema kuwa wanapoanza safari ya miaka 20 ijayo wamedhamilia kuongeza kasi ya mageuzi katika kuifanya mahakama iwe ya kisasa zaidi,yenye uwazi zaidi na yenye uwajibikaji wa hali ya juu.
“Tunatarajia kuendelea na miradi ya ujenzi na ukarabati hasa katika mahakama za wilaya na mahakama za mwanzo,pamoja na kuimarisha upatikanaji wa haki kwa makundi maalumu”alisema
Aidha alielezea shughuli zitakazofanywa kuelekea maadhimisho ya miaka 20 ya mahakama kuu kanda ya Iringa ambayo yanatarajiwa kufanyika disemba 15, 2025 ni pamoja na utoaji wa elimu kwa njia ya redio na televisheni.
Alisema kuwa mada zitakazo zungumziwa ni pamoja na taratibu za kufungua mashauri ya mirathi,uandishi wa wosia na umuhimu wake,ukatili wa kijinsia,utatuzi wa migogoro ikiwemo ya ardhi na madai.
“Tutatoa elimu kwa wananchi pia katika masuala ya takala na ndoa, uendeshaji wa mashauri kwa njia ya kielektroniki,haki za mtoto na ulinzi wa mtoto,pamoja na utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi”alisema Jaji






0 Comments