MOSHI.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro kimewaasa viongozi wa dini nchini kuhubiri amani na kukemea vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyofanywa katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika mitandao ya kijamii kwani amani ya Tanzania italindwa na Watanzania wenyewe.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Katibu wa Siasa na Itikadi na Uenezi mkoa wa Kilimanjaro, Abrahamu Urio alipozungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM mkoa ambapo alisema kuwa, kila Mtanzania anawajibu wa kuhakikisha anailinda amani na kukemea vikali vitendo vyenye viashiria vya uvunjifu wa amani.
"Viongozi wa Dini ninyi ni watu muhimu katika Taifa hivyo niwasihi sana tuubiri amani yetu na kukemea vikali yale yote yanayofanywa kwa lengo la kuvuruga amani yetu pamoja na kuwaelimisha vijana kutambua umuhimu wa amani yetu" Alisema Urio.
Alisema kuwa, viongozi hao wa Dini hawapaswi kusubiria mpaka damu imwagike au wananchi kujeruhiana ndipo waje kukemea matendo hayo na badala yake wanapaswa kuchukua tahadhari mapema.






0 Comments