Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA Amosi Makalla
ameipongeza TRA kwa kuendelea kutoa Elimu ya kodi kwa wafanyabiashara, huku akisisitiza umuhimu wa kuanzishwa kwa jukwaa maalum la wadau kutoka sekta mbalimbali ili kukuza uelewa wa pamoja na kuongeza mapato ya Serikali.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mhe. Makalla akiwa ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Ndg. Misaile Mussa amesema ziara hiyo imefanyika kama sehemu ya juhudi za kuimarisha mahusiano kati ya TRA na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato Mkoani hapo.
Aidha CPA. Makalla ameishukuru TRA kwa kuendelea kuboresha mifumo na huduma za kielektroniki ambapo amebainisha kuwa maboresho hayo yamerahisisha ulipaji kodi kwa wakati na kuongeza ufanisi katika utoaji wa Huduma.
Kwa upande wake Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha Bw. Deogratius Shuma ameahidi kushughulikia changamoto zinazowakabili walipakodi kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali hatua itakayosaidia kujenga taswira chanya ya taasisi na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.








0 Comments