Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amefutia mashtaka na kumwachia huru mfanyabiashara wa vipodozi Jenifer Jovin (26) maarufu Niffer na Mika Lucas Chavala, waliokuwa na kesi ya uhaini.
Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Desemba 3, 2025 na Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya, baada wakili wa Serikali, Titus Aron kuileleza Mahakama hiyo kuwa DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao wawili.
DPP amewafutia kesi hiyo ya uchunguzi namba 26388/ 2025 chini ya kifungu namba 92(1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai, Sura ya 20 ilivyofanya marejeo mwaka 2023.
"Mahakama inakubaliana na ombi la upande wa Jamhuri kama lilivyowasilishwa, hivyo inawaachua huru washtakiwa hawa wawili," amesema Hakimu Lyamuya.





0 Comments