Header Ads Widget

WAZIRI KIJAJI ASISITIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA UHIFADHI.

 


Na,Jusline Marco:Karatu.Arusha


TAASISI za uhifadhi zimetakiwa kuimarisha matumizi ya teknolojia za kisasa katika uhifadhi na ulinzi wa rasilimali za wanyamapori ili kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori.


Waziri wa Maliasili na utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ametoa maelekezo hayo leo Novemba,28,2025 wakati alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro katika ziara yake ya kujitambulisha kwenye taasisi na kukagua utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo.


Katika kikao hicho Waziri Kijaji  ameelekeza kuwa kila taasisi ni lazima iwekeze kwenye teknolojia za kısasa ili kuimarisha ulinzi wa rasilimali za nchi ambazo ni kichocheo cha wageni mbalimbali kutembelea nchi yetu.



Kwa upande wake naibu waziri wa wizara hiyo Mhe.Hamad Hassan Chande amewataka watumishi katika sekta ya uhifadhi na utalii kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na ubunifu katika kuwahudumia wageni.



Naye Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi wakati akiwatambulisha viongozi hao kwa menejimenti ya Ngorongoro,amewataka watumishi wa mamlaka hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuharakisha mipango ya serikali inatekelezwa.


Mwisho.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI