NA HADIJA OMARY
LINDI.....Utekelezaji wa miradi ya mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Lindi umeendelea kuleta mabadiliko chanya katika jamii, ikiwamo kuwajengea wananchi uwezo wa kubaini changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi kupitia miradi ya maendeleo wanayoibua wao wenyewe.
Akizungumza Katika kikao kazi kilichowakitanisha walagbishi kutoka Katika vijiji 10 vya halmashauri ya Mtama vinavyotekeleza Mradi huo kilichofanyika huko manispaa ya Lindi mwakilishi wa Shirika la TWAWEZA EAST AFRICA Richard Temu Amesema Mradi huo wa Ulagbishi umekuwa na lengo mahususi la kuhakikisha wananchi wanakuwa mstari wa mbele katika kupanga, kuibua na kutekeleza vipaumbele vyao, hatua inayowasaidia kujenga jamii yenye uelewa na ushiriki unaoleta matokeo chanya ya muda mrefu.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa mashirika ya mtandao wa NGO'S (LANGO) Mkoa wa Lindi Bi.Aina Pero Amesema Mradi huo wa Ulagbishi unafanywa kwa mashirikiano ya Shirika Lao pamoja na TWAWEZA EAST AFRICA kuanzia mwaka 2022. Ambapo Utekelezaji wake unahusisha vijiji 10 vya halmashauri ya Mtama
Alivitaja vijiji vilivyofikiwa na Mradi huo ni pamoja na Nahuka huka, Chiuta, Mmumbu, Sudi, Mandawa , Mtua longa, Mtakuja , Mwangu, Rondo na Namangale
Amesema Katika kipindi chote cha Utekelezaji wa Mradi huo umejikita katika kuwajengea uwezo wananchi, hususan katika maeneo ambayo awali wananchi hawakuwa na uelewa mpana juu ya nafasi yao katika kuchochea maendeleo.
Amesema Mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa kwa wananchi kupata mwamko mpya wa ushiriki wa maendeleo ambapo Matatizo mbali mbali yaliibuliwa na kufanyiwa kazi
Baadhi ya wananchi wamesema mradi huo umeongeza uelewa wao juu ya umuhimu wa kuibua vipaumbele na kutengeneza miradi ya maendeleo bila kusubiri serikali kuchukua hatua ya awali.
Wameeleza kuwa baada ya kukamilisha hatua ya uibuaji wa miradi, Serikali imekuwa ikiunga mkono jitihada hizo kwa kupeleka fedha za kumalizia baadhi ya miradi waliyoianzisha wenyewe, jambo lililoongeza hamasa ya ushiriki wa wananchi kwenye kupanga na kutekeleza mipango ya kijamii.
0 Comments