Header Ads Widget

WATU TISA WAFARIKI DUNIA WAKATI URUSI IKIISHAMBULIA UKRAINE USIKU KUCHA- ZELENSKY

 

Watu tisa wameuawa katika mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine usiku kucha, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema.

Urusi ilirusha zaidi ya ndege zisizo na rubani 470 na makombora 47 katika "shambulio hilo lisilo na aibu", aliandika katika chapisho kwenye Telegram.

Wilaya tatu za mji wa pili wa Ukraine, Kharkiv, zilipigwa na shambulio kubwa la ndege zisizo na rubani ambalo lilijeruhi zaidi ya watu 30, wakiwemo watoto.

Picha zilizochapishwa mtandaoni zilionesha majengo na magari yakiwaka moto. Kukatika kwa umeme kunaathiri maeneo kadhaa kote nchini, wizara ya nishati ya Ukraine ilisema.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI