Header Ads Widget

TRUMP AMTETEA MWANA WA MFALME WA SAUDIA KUHUSU MAUAJI YA KHASHOGGI

 

Rais wa Marekani Donald Trump amesema Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman "hakujua chochote" kuhusu mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi mwaka 2018, alipomkaribisha mtawala wa ufalme huo katika Ikulu ya White House.

Maoni ya Trump yalionekana kupingana na tathmini ya kijasusi ya Marekani mwaka 2021 ambayo ilisema kwamba mwanamfalme huyo alikuwa ameidhinisha operesheni iliyosababisha kifo cha Khashoggi katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia huko Istanbul mwaka 2018.

Mwanamfalme huyo, ambaye amekana shutuma dhidi yake, alisema katika Ikulu ya White House kwamba Saudi Arabia "ilifanya mambo yote sahihi" kuchunguza kifo cha Khashoggi, ambacho alikiita "kibaya".

Ilikuwa ziara yake ya kwanza ya Marekani tangu mauaji hayo, ambayo yalisababisha mshtuko katika uhusiano kati ya Marekani na Saudi Arabia.

Katika Ofisi ya Oval siku ya Jumanne, Trump alimjibu mwandishi wa habari aliyeuliza swali kuhusu mauaji hayo. "Unamtaja mtu aliyekuwa na utata sana," rais wa Marekani alisema. "Watu wengi hawakumpenda bwana huyo unayemzungumzia. Iwe unampenda au humpendi, mambo hutokea." "Lakini yeye hakujua lolote kuihusu," Trump aliongeza.

"Huna haja ya kuwaaibisha wageni wetu." Mwanamfalme aliongeza kuwa Saudi Arabia "ilifanya hatua zote sahihi" kuchunguza mauaji hayo, ambayo aliyaita "mabaya" na "makosa kubwa".

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI