Header Ads Widget

WALIMU MWANZA WAASWA KUEPUKA MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO


Na Chausiku Said 

Matukio Daima Mwanza.

Walimu Mkoani Mwanza wametakiwa kufanya kazi kwa uweledi na kuepuka matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yenye kuleta taharuki katika jamii huku wakitakiwa kushikamana na kufanya kazi kwa kufata maadili na kutanguliza mbele maslahi ya jamii na Taifa kwa ujumla.


Rai hiyo imetolewa jana Novemba 19 na mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Tanzania Mkoa wa Mwanza (CWT) Sholi Maduhu alipokuwa akikabidhi viti 20 kwa walimu wa shule ya msingi Nyashana Wilayani Nyamagana kutokana na changamoto ya ukosefu wa viti uliokuwa ukiwakabili walimu hao.


Maduhu ameeleza kuwa uwepo wa viti hivyo vitawasaidia walimu kuandaa kazi vizuri huku akiwasisitiza  kuwa kwa asilimia kubwa mazingira wanayofanyia kazi walimu ni mazuri, japo ofisi zao zinasaulika katika swala la miundombinu ya ndani.

Maduhu ameeleza kuwa taasisi ya Chama Cha Walimu Tanzania pamoja na kazi za msingi za utetezi ni lazima kufahamu wajibu wa mwalimu anatimiza kwa kufahamu changamoto mbalimbali wanazopitia.

"Mimi kama mwenyekiti wa Mkoa wa Mwanza mwezi wa nane niliitwa hapa kuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya darasa la saba na katika risala yao moja kati ya changamoto walioeleza walimu wa Nyashana shule ya msingi ni ukosefu wa viti vya walimu," alisema Maduhu.

Suzana Abigael, Silvia Shawishi na Simon Masalu ni baadhi ya walimu kutoka shule hiyo ambao wameeleza kuwa wamekuwa na changamoto hiyo ya ukosefu wa viti hali iliyowapelekea kukaa kwenye madawati ya wanafunzi, hivyo uwepo wa viti hivyo vitawahamasisha walimu hao kufanya kazi zao kwa bidii.

" Tunawashukuru viongozi wa CWT Mkoa wa Mwanza kwa kutukumbuka kutuletea viti hivi kwani vitawahamasisha walimu kufanya kazi zao kwa bidii na uweledi," walisema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI