NA MATUKIO DAIMA MEDIA, LINDI
Diwani Mteule wa Kata ya Mtanda Jimbo la Manispaa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Mheshimiwa Idd Lulida amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho kugombea Nafasi ya Umeya Katika Manispaa hiyo
Fomu hiyo amechukua Leo November 20, 2025 Katika ofisi ya Chama Mkoa zilizopo Wailes katika manispaa ya Lindi na kukabidhiwa fomu na Katibu wa chama hicho Wilaya ya Lindi bwana Mohammed Lawa
Mhe Lulida amesema dhamira yake kuu ya kuomba ni kujielekeza katika kuboresha huduma muhimu za msingi kama elimu,barabara,afya na kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji sambamba na maandalizi ya kupokea miradi mikubwa ya kimkakati kama iliyoainishwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025-30 na kuitekeleza kwa pamoja kwa maendeleo ya Wananchi wa Manispaa ya Lindi.







0 Comments