Header Ads Widget

WAGENI ZAIDI YA 500 WAHUDHURIA KONGAMANO LA DINI ARUSHA, WASIFU AMANI NA UTULIVU

 

Wakaribisha wengine nchini wakiwataka kuachana na upotoshaji wa Mtandaoni

Zaidi ya Wageni 500 kutoka kwenye Mataifa mbalimbali ya Barani Afrika na nje ya Afrika wamekutana kwa siku mbili Mkoani Arusha kwenye Kongamano la kujadili kuhusu mchango wa dini katika uchumi na maendeleo, wengi wakifurahia amani na utulivu walioushuhudia nchini tangu kuwasili kwao siku tano zilizopita.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti, miongoni mwa washiriki hao kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na nchini Senegal, wameeleza kuwa Kongamano hilo lilitaka kuahirishwa kutokana na kile walichokuwa wakikiona kwenye Mitandao ya Kijamii.

"Wakati tunakuja Tanzania tulisikia vitu vingi, tukaangalia kwenye runinga na tukaona habari za uwepo wa machafuko, tukawa na wasiwasi wa Kongamano letu kiasi cha kuanza kufikiria kuahirisha lakini tunamshukuru Mungu tumefika na tumekuta amani ya kutosha na Mungu ni mwema sana kwasababu amewezesha amani Tanzania, tunamshukuru sana Mungu." Amesema Joela Athumani, Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.


Bi Joela amewataka watanzania kuishikilia kwa nguvu baraka ya amani waliyobarikiwa na Mwenyenzi Mungu, akiwataka wale wote waliokuwa wamepanga kuja nchini kutokuwa na wasiwasi wowote wa kiusalama kwani hali ni shwari na shughuli zinaendelea kama kawaida.


Kwa upande wake Bw. Ogi Kabongo, Mkazi wa Kinshasa nchini DRC,  ameeleza athari za ukosefu wa amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, akiwataka Watanzania kudumisha amani ya Tanzania kwa gharama yoyote ile kwani ukosefu wa amani unadhorotesha na kuua kabisa ustawi na maendeleo ya wananchi.


Aidha Bw. Fransis Owusu, Raia wa Senegal na Rais wa Full Gospel Business Men's Fellowship International ameitaka Jamii kuendelea kuiombea amani ya Tanzania, akisema amani hiyo mara zote imekuwa msingi muhimu wa maendeleo na kiwezeshi kikubwa cha mafanikio katika shughuli za kiuchumi







TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI