Header Ads Widget

VIJANA WAPONGEZA HOTUBA YA RAIS SAMIA BUNGENI, WAAHIDI USHIRIKIANO KWA NANAUKA

 


Na Matukio Daima Media

SAID Mkono, Mkazi wa Dar Es Salaam ameeleza kufurahishwa na dhamira njema ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kushughulikia changamoto za Vijana kwa kuunda Wizara ya Maendeleo ya Vijana nchini, akisema wizara hiyo itaenda kuondoa kero na malalamiko waliyokuwa nayo Vijana.


Wakati wa hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge la Tanzania, Rais Samia alieleza dhamira yake ya kuunda Wizara mpya ya Maendeleo ya Vijana na siku chache baadae alipotangaza baraza la Mawaziri kati ya Wizara 27 alizozitangaza Viongozi wake, alimtaja Mhe. Joel Nanauka kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Maendeleo ya Vijana ambaye atasimamia Wizara hiyo chini ya wasaidizi kadhaa kutoka Ofisi ya Rais.


Akiisifu hotuba ya Rais Samia Bungeni na kuonesha matumaini makubwa ikiwa aliyoyasema yatatekelezwa, Mkono amemshukuru Rais Samia kwa kuunda Wizara hiyo, akiomba Viongozi watakaosimamia Wizara hiyo chini ya Waziri Nanauka kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha matokeo chanya yanapatikana kwa Vijana.


Kauli ya Rais Samia na hali ya mtanziko iliyokuwepo kutokana na matukio ya uvunjifu wa amani yaliyoibua vurugu siku ya uchaguzi Oktoba 29 na siku zilizofuata, kundi la vijana likitajwa kuongoza, zilifanya wengi kusubiri kwa hamu kuundwa kwa wizara hiyo lakini pia kujua atakayeiongoza pamoja na majukumu yaliyoko mbele yake.

Mtaalamu wa saikolojia na mwezeshaji, Charles Nduku amenukuliwa akizungumza na Vyombo vya habari akisema eneo kubwa ambalo Waziri Nanauka anapaswa kulishughulikia ni pamoja na kubadili mtazamo wa vijana juu ya wanavyotazama fursa na kuwaonyesha vitu vya kufanya, kwani Tanzania ni tajiri, lakini vijana wanakosa maarifa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI