
Mtaalam wa Dijitali katika elimu kutoka Shirika la Maendeleo la serikali ya Ubelgiji (ENABEL), Lotte Van Praet akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi seti 27 za Computer mpakato, mfumo wa umeme jua na Projector vinavyotumika kufundishi kidijitali kwa halmashauri tatu za mkoa Kigoma zenye thamani ya shilingi milioni 81 zilizotolewa na shirika hilo
Mtaalam wa Dijitali katika elimu kutoka Shirika la Maendeleo la serikali ya Ubelgiji (ENABEL), Lotte Van Praet akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi seti 27 za Computer mpakato, mfumo wa umeme jua na Projector vinavyotumika kufundishi kidijitali kwa halmashauri tatu za mkoa Kigoma zenye thamani ya shilingi milioni 81 zilizotolewa na shirika hilo
Mkuu wa mkoa Kigoma Simon Sirro akizungumza katika hafla ya kukabidhi seti 27 za Computer mpakato vitakazotumika kufundishia kidijitali katika shule za sekondari mkoani Kigoma zilizotolewa na Shirika la maendeleo la serikali ya Ubelgiji (ENABEL) na kukabidhiwa kwa halmashauri tatu za mkoa Kigoma.
Mtaalam wa Dijitali katika elimu kutoka Shirika la Maendeleo la serikali ya Ubelgiji (ENABEL), Lotte Van Praet (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Mkuu wa mkoa Kigoma Simon Sirro (wa pili kushoto) na Katibu Tawalaa wa mkoa Kigoma Hassan Rugwa (kushoto) kuhusu seti 27 za Computer mpakato, mfumo wa umeme jua na Projector vinavyotumika kufundishi kidijitali masomo mbalimbali kwa shule za sekondari mkoani Kigoma vilivyokabidhiwa kwa halmashauri tatu za mkoa Kigoma
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
MKOA Kigoma unaelezwa kupiga hatua kubwa katika matumizi ya kidijitali katika kufundishia hali iliyoufanya mkoa huo kufanya vizuri kitaaluma katika mitihani mbalimbali ya Kitaifa kwa shule za sekondari nchini.
Katibu Tawala wa mkoa Kigoma,Hassan Rugwa alieleza hayo wakati Mkuu wa mkoa Kigoma,Balozi Simon Sirro akikabidhi kwa Wakurugenzi wa halmashauri tatu za mkoa Kigoma jumla ya seti 27 za Computer mpakato, Projector, mfumo wa umeme jua na vifaa vingine vinavyosaidia katika kujifunza na kufundishia vilivyotolewa na Shirika la Maendeleo la serikali ya Ubelgiji (ENABEL) ili kuchochea ufundishaji wa kidijitali mkoani Kigoma.
Katibu Tawala huyo wa mkoa Kigoma alisema kuwa ufundishaji kwa njia ya Computer kidijitali umechochea mkoa Kigoma kutoa shule mbili katika shule 10 bora zilizofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha nne mwaka uliopita kwa shule za serikali .
Sambamba na hilo Katibu Tawala huyo wa mkoa Kigoma alisema kuwa kwa kutumia mfumo huo mkoa umeweza kuongoza kwa kutoa mwanafunzi bora wa somo la Kemia, kushika namba mbili kitaifa somo la Fizikia huku ikishika namba tatu katika somo la Hisabati na kwamba mkoa umejipanga kuhakikisha inaongeza matumizi ya computer kidijitali katika kufundishia na kujifunzia.
Akikabidhi vifaa hivyo MKUU wa mkoa Kigoma, Balozi Simon Sirro amewataka wakurugenzi wa halmshauri za mkoa Kigoma kuongeza nguvu katika kukuza na kuimarisha matumizi ya mfumo wa computer kidijitali katika ufundishaji kwa walimu na ujifunzaji kwa wanafunzi ili kuongeza ufaulu na kuongeza ari ya wanafunzi katika kujifunza.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa dunia inapoelekea sasa matumizi ya teknolojia ya habari na mawasilianao ndiyo imechukua nafasi hivyo kuwepo kwa mpango wa kujifunza na kufundishia kidijitali kunawapa nafasi wanafunzi kujiandaa kuingia kwenye ushindaji wa ajira wenye ujuzi.
Awali Mtaalam wa Dijitali katika elimu kutoka Shirika la Maendeleo la serikali ya Ubelgiji (ENABEL), Lotte Van Praet alisema kuwa shirika hilo limekabidhi seti 27 za Computer mpakato,Projector na mfumo wa umeme jua zenye thamani ya shilingi milioni 81 ambazo zitatumika kwenye shule 12 za sekondari na vituo vitatu vya mafunzo endelevu kwa walimu (TRC) kwenye halmashauri tatu za mkoa Kigoma.










0 Comments