Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ,Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji mstaafu Mathew Mwaimu alisema matukio hayo hayapaswi kuungwa mkono kwa sababu yanavunja amani katika nchi na kuvunja usalama wa wananchi.
Amesema kutokana na matukio hayo, tume imepanga kufanya uchunguzi wa kina. “Tumekwishajipanga katika jambo hilo ili tuweze kuona ni maeneo yapi ambayo kwa kuangalia matukio yaliyojitokeza tume inaweza kutoa ushauri kwa serikali na vyombo vingine kwa madhumuni ya kutaka kuendelea kulinda amani katika nchi yetu,” alisema. Jaji
Mwaimu amesema matukio yaliyojitokeza yamevunja baadhi ya haki za wananchi kwa sababu wamepoteza maisha na wengine wamepoteza mali. Alisema tume imeona matukio hayo yanapaswa kufanyiwa uchunguzi wa kina ili waweze kutoa ushauri namna ya kuondokana na matatizo ya namna hiyo miaka mingine ya uchaguzi.







0 Comments