Header Ads Widget

TANGU KIPINDI CHA UCHAGUZI MKUU HADI SASA IDADI YA WATALII YAFIKIA 12000.

 

Na,Jusline Marco;Arusha

Afisa Uhifadhi Mkuu Idara ya huduma za Utalii na Masoko Ngorongoro Bw. Peter Makutian amesema tangu kipindi cha uchaguzi mkuu hadi kufikia Novemba 5 mwaka huu takribani wageni 12000 kutoka mataifa mbalimbali wameendelea kutembelea hifadhi ya Ngorongoro na kufanya Utalii.

Akizungumza katika geti kuu la kuingia hifadhi ya Ngorongoro, Bwn.Makutian amesema Wageni kutoka mataifa mbalimbali wanaotembelea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na kuendelea kufanya shughuli za utalii kwa amani, usalama na utulivu na kufurahia vivutio mbalimbali vya utalii vilivyoko hifadhi hiyo.

 “Ngorongoro  tunaendelea kupokea wageni  katika kipindi hiki cha msimu wa wastani na tuna Imani kuelekea kipindi cha sikukuuu za mwisho wa mwaka watalii watakuwa wengi zaidi .” alisema Makutian.

Naye mmoja wa wageni  kutoka Nchini Colombia Isabella Jerónimol  ameeleza kuwa ametembeleaa Tanzania akiwa na familia ya watu 26 ambapo chaguo lao  ni kuona hifadhi ya Ngorongoro kutokana na hali ya utulivu, amani, ukarimu pamoja na utajiri wa vivutio vya utalii vilivyopo.

Wakati huohuo Bw. Dunstan Sospeter kutoka jijini Dar es Salaam akiwa katika hifadhi ya Ngorongoro na Familia yake ameelezea kufurahishwa na hali ya usalama na kushuhudia utalii wa wanyamapori, uhifadhi endelevu, Wanyama mbalimbali ambao wanaweza kuonekana kwa pamoja katika muda ambapo pia ametumia fursa hiyo  na familia yake kutembelea  Bonde la Olduvai, mchanga unaohama na kreta ya Ngorongoro.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI