Header Ads Widget

TANAPA YASHIRIKI SEMINA JUU YA UTUNZAJI MAZINGIRA KIMATAIFA, KUPUNGUZA HEWA UKAA


Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) leo Novemba 28, 2025 jijini Arusha limeshiriki semina ya siku moja iliyoendeshwa na Taasisi ya kimataifa EY (Ernst & Young) ambayo inajihusisha na ukaguzi, ushauri wa kodi na ushauri wa kimkakati.

Semina hiyo ililenga kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa viwango vya kimataifa ambayo imedhamiria kupunguza hewa ya ukaa kulinganana shughuli zinazofanywa na binadamu.

TANAPA kama mdau mkubwa wa mazingira ina jukumu la kuandaa mbinu na mikakati madhubuti ya kupambana na uchafuzi wa mazingira.

TANAPA inaendelea kuwekeza kwenye matumizi ya vitendea kazi ambavyo ni rafiki kwa mazingira, mifumo ya kisasa inayosaidia kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa ili kuongeza tija kwenye kulinda usalama wa mazingira ya wanyamapori na mimea.

Semina hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa  TANAPA, ikihusisha Makamishana wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania wakiongozwa na Kamishna wa Uhifadhi TANAPA Mussa Nassoro Kuji.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI