Header Ads Widget

“SPORT FISHING” INAYOFANYIKA KATIKA ZIWA LENYE KINA KIREFU ZAIDI AFRIKA - MAHALE NDIO HABARI YA MJINI


Na. Jacob Kasiri - Mahale.


“Sport fishing” kando kando ya Ziwa Tanganyika ndani ya Hifadhi ya Taifa Milima Mahale ni miongoni mwa zao la utalii linalochipua kwa kasi na kuongeza hamasa kwa watalii kutembelea hifadhi hiyo iliyopo Magharibi mwa Tanzania. Utalii huu yumkini unaofanyika katika hifadhi zenye maziwa na mito unaendelea kushika kasi na kutoa uzoefu wa kipekee kwa watalii wenye shauku na  ari ya kuvua samaki katika ziwa lenye kina kirefu duniani.

Kinachowavutia watalii ndani ya Hifadhi ya Taifa Milima Mahale ni utulivu wa mazingira ya hifadhi, mandhari ya kipekee ya ziwa Tanganyika, mpangilio wa safu za milima, upepo mwanana kutoka Ziwa Tanganyika unaoungana na ule unaotoka katika misitu ya Mahale yenye asili ya Miombo na Kikongo kwa mbali ambayo hutengeneza upepo mwanana usio na baradi wala joto. 

Mchanganyiko wa pepo hizo humfanya mtalii ajihisi kama yuko ndani ya bustani ya Eden inayonenwa na vitabu vitakatifu.



Aidha, katika mahojiano na mwandishi wa makala hii, watalii hao “walijimwayamwaya” na kusema uzoefu wao wa safari za kitalii usioathiriwa na matukio ya muda mfupi, ndio uliowasukuma kuja kutalii katika hifadhi hii inayosimamiwa na TANAPA.

Kwa sasa, “sport fishing” katika Ziwa Tanganyika inaendelea kuwa kivutio kinachopendwa zaidi na watalii wengi wanaozuru hifadhi hiyo, huku wakichagizwa na utulivu, utalii wa sokwe sanjari na kushuhudia jua likizama Magharibi mithili ya kuishilia ndani ya Ziwa Tanganyika.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI