Na Fadhili Abdallah,Kigoma
MKUU wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro amewataka wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya kati mkoani Kigoma kuongeza kasi katika kujifunza computer na matumizi sahihi ya vifaa hivyo kwani vina mchango mkubwa katika maisha yao ya baadaye
Balozi Sirro ametoa rai hiyo akikabidhi sehemu ya computer 50 kwa chuo cha ufundi Stadi (VETA) Kigoma ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake kwa chuo hicho alipofanya ziara chuoni hapo na kukuta uwepo wa changamoto wa vifaa hivyo katika kujifunza na kufundishia.
Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro akikabidhi sehemu ya Computer 50 alizoahido kutoa kwa Chuo Cha Ufundi Stadi (VETA) Kigoma
Mkuu huyo wa mkoa Kigoma alisema kuwa kwa sasa dunia imeelekea katika matumizi ya Computer kwa sehemu kubwa ya maisha ya binadamu, shughuli za utendaji na mipango ya maendeleo na kwamba matumizi sahihi ndiyo yatayowavusha vijana katika mipango yao ya maendeleo.
Aidha Mkuu huyo wa mkoa amevitaka vyuo vya kati vya elimu mkoani Kigoma kusisitiza ufundishaji elimu ya Computer kuwezesha wahitimu wa vyuo hivyo kuwa na uelewa wa juu wa matumizi ya vifaa hivyo ili kuwasaidia katika shughuli zao mbalimbali baada ya kumalizi masomo.





0 Comments